Skip to content
Orodha ya Sura /

الحَاقة

الحَاقة is chapter 69 of the Quran and has 52 verses. This page presents it in full in the Uthmani script, with a verse-by-verse translation of its meaning.

52 Aya Sura Na. 69
Nenda kwenye aya
Kiswahili · Barawani
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

ٱلۡحَآقَّةُ

Tukio la haki.

Explanation & meanings · 1
  1. Kiyama ni Tukio litakalo tukia kwa haki, yaani kwa kweli.

مَا ٱلۡحَآقَّةُ

Nini hilo Tukio la haki?

Explanation & meanings · 1
  1. Nini hicho Kiyama kitacho tokea kweli?

وَمَآ أَدۡرَىٰكَ مَا ٱلۡحَآقَّةُ

Na nini kitakujuulisha nini hilo Tukio la haki?

Explanation & meanings · 1
  1. Na kitu gani kitacho kujuvya ukweli wake, na kitacho kupa sura ya kitisho chake na shida zake?

كَذَّبَتۡ ثَمُودُ وَعَادُۢ بِٱلۡقَارِعَةِ

Thamudi na A'di waliukadhibisha Msiba unao situsha.

Explanation & meanings · 1
  1. Kina Thamudi na kina A'di walikanusha Kiyama kinacho wagutua walimwengu wote kwa kitisho chake na shida zake.

فَأَمَّا ثَمُودُ فَأُهۡلِكُواْ بِٱلطَّاغِيَةِ

Basi Thamudi waliangamizwa kwa balaa kubwa mno.

Explanation & meanings · 1
  1. Ama Thamudi basi walihilikiwa kwa tukio lilio pindukia mipaka yote kwa ukali wake.