Skip to content
Orodha ya Sura /

نُوح

نُوح is chapter 71 of the Quran and has 28 verses. This page presents it in full in the Uthmani script, with a verse-by-verse translation of its meaning.

28 Aya Sura Na. 71
Nenda kwenye aya
Kiswahili · Barawani
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

إِنَّآ أَرۡسَلۡنَا نُوحًا إِلَىٰ قَوۡمِهِۦٓ أَنۡ أَنذِرۡ قَوۡمَكَ مِن قَبۡلِ أَن يَأۡتِيَهُمۡ عَذَابٌ أَلِيمٞ

Hakika Sisi tulimtuma Nuh'u kwa watu wake: Uwaonye kaumu yako kabla ya kuwafikia adhabu chungu.

Explanation & meanings · 1
  1. Hakika Sisi tulimtuma Nuh'u kwa watu wake, na tukamwambia: Waonye watu wako kabla haijawajia adhabu yenye machungu makali.

قَالَ يَٰقَوۡمِ إِنِّي لَكُمۡ نَذِيرٞ مُّبِينٌ

Akasema: Enyi watu wangu! Kwa hakika mimi ni mwonyaji wa dhaahiri kwenu!

Explanation & meanings · 1
  1. Nuh'u akasema: Enyi watu wangu! Hakika mimi ni mwonyaji kwenu, nina risala kutoka kwa Mola wenu Mlezi kwa lugha mnayo ijua,

أَنِ ٱعۡبُدُواْ ٱللَّهَ وَٱتَّقُوهُ وَأَطِيعُونِ

Ya kwamba mumuabudu Mwenyezi Mungu, na mumche Yeye, na mumt'ii.

Explanation & meanings · 1
  1. Ya kwamba mumt'ii Mwenyezi Mungu, na mumnyenyekee katika kutimiza waajibu zote; na mwogopeni Yeye kwa kuacha mnayo katazwa, na nit'iini mimi katika ninayo kunasihini.

يَغۡفِرۡ لَكُم مِّن ذُنُوبِكُمۡ وَيُؤَخِّرۡكُمۡ إِلَىٰٓ أَجَلٖ مُّسَمًّىۚ إِنَّ أَجَلَ ٱللَّهِ إِذَا جَآءَ لَا يُؤَخَّرُۚ لَوۡ كُنتُمۡ تَعۡلَمُونَ

Atakughufirieni madhambi yenu, na atakuakhirisheni mpaka muda ulio wekwa. Hakika muda wa Mwenyezi Mungu utapo fika haucheleweshwi. Laiti mngejua!

Explanation & meanings · 1
  1. Ndipo Mwenyezi Mungu atapo kusameheni madhambi yenu, na atakupeni umri mrefu mpaka ifike ajali iliyo wekwa mwisho wa umri wenu. Hakika mauti yakija hayaakhirishwi kabisa! Lau kuwa mngeli jua majuto mtakayo kuwa nayo utapo kwisha muda wenu mngeli amini.

قَالَ رَبِّ إِنِّي دَعَوۡتُ قَوۡمِي لَيۡلٗا وَنَهَارٗا

Akasema: Ee Mola wangu Mlezi! Hakika mimi nimewaita watu wangu usiku na mchana!

Explanation & meanings · 1
  1. Nuh'u akasema: Mola wangu Mlezi! Hakika mimi nimewaita watu wangu waamini usiku na mchana bila ya kuchoka,