Akitwaharika mwanamke baada ya swala ya Alfajiri, je ajizuie na afunge swaumu siku hiyo?, na je siku hiyo itahesabika kwake kuwa kafunga au atatakiwa kuilipa siku hiyo?
السؤال
Swali la 1:
Akitwaharika mwanamke baada ya swala ya Alfajiri, je ajizuie na afunge swaumu siku hiyo?, na je siku hiyo itahesabika kwake kuwa kafunga au atatakiwa kuilipa siku hiyo?
س1: إذا طهرت الـمرأة بعد الفجر مباشرةً فهل تمسك وتصوم هذا اليوم، ويكون يومها لها، أو عليها قضاء ذلك اليوم؟
الجواب
Jawabu la 1:
Akitwaharika mwanamke baada ya kuchomoza Alfajiri, wanachuoni wana kauli mbili juu ya mwanamke huyu katika kujizuia kula na kunywa na tendo la ndoa mchana wa siku hiyo.
Kauli ya kwanza: Atalazimika kujizuia kula, kunywa, na tendo la ndoa katika masaa yaliyobakia kwa siku hiyo, lakini haitohesabika kwake siku hiyo, bali atawajibika kuilipa, na hii ndio kauli ya wanachuoni wengi katika madhehebu ya Imam Ahmad -Allah amrehemu-
Kauli ya pili: Hatolazimika kujizuia kula, kunywa, na tendo la ndoa mchana wa siku hiyo, kwa sababu haikubaliki funga kwa siku hiyo, kwa sababu mwanzo wa siku alikuwa kwenye hedhi, na aliye katika hedhi hafai kufunga, na kwakuwa swaumu yake si sahihi, basi hakuna faida ya kujizuia kula, kunywa, na tendo la ndoa, na wakati wa siku hiyo si wakati wa kuheshimiwa kwa upande wake, kwa sababu ameamrishwa kula mwanzo wa mchana, bali ni haramu kwake kufunga mwanzo wa mchana,
Na swaumu ya kisheria: Ni kujizuia na vyote vyenye kufunguza kwa lengo la kumwabudu Allah toka kuchomoza Alfajiri mpaka kuzama kwa jua.
Na kauli hii -kama unavyoiona- ina nguvu zaidi kuliko kauli ya kwanza ya kujizuia, lakini kwa kauli zote hizi mbili itamlazimu kulipa siku hii.
ﺟ1: إذا طهرت المرأة بعد طلوع الفجر فللعلماء في إمساكها ذلك اليوم قولان:
القول الأول: أنه يلزمها الإمساك بقية ذلك اليوم، ولكنه لا يحسب لها، بل يجب عليها القضاء، وهذا هو المشهور من مذهب الإمام أحمد رحمه الله.
والقول الثاني: أنه لا يلزمها أن تمسك بقية ذلك اليوم؛ لأنه يومٌ لا يصحّ صومها فيه؛ لكونها في أوله حائضًا ليست من أهل الصّيام، وإذا لم يصح لم يبق للإمساك فائدةٌ، وهذا الزمن زمنٌ غير محترمٍ بالنّسبة لها؛ لأنها مأمورةٌ بفطره في أول النهار، بل محرمٌ عليها صومه في أول النهار،
والصوم الشرعيّ: هو الإمساك عن المفطّرات تعبّدًا لله عز وجل من طلوع الفجر إلى غروب الشمس.
وهذا القول -كما تراه- أرجح من القول بلزوم الإمساك، وعلى كلا القولين يلزمها قضاء هذا اليوم.