Skip to content

Atakapotwaharika aliyekuwa na hedhi, na akaoga josho kubwa baada ya swala ya Alfajiri, na akaswali, na akaikamilisha swaumu ya siku yake ile, je anawajibika kulipa siku hiyo?

السؤال

Swali la 1:

Atakapotwaharika aliyekuwa na hedhi, na akaoga josho kubwa baada ya swala ya Alfajiri, na akaswali, na akaikamilisha swaumu ya siku yake ile, je anawajibika kulipa siku hiyo?

س2: إذا طهرت الحائض، واغتسلت بعد صلاة الفجر، وصلت، وكملت صوم يومها، فهل يجب عليها قضاؤه؟

الجواب

Jawabu la 1:

Atakapo twaharika Mwanamke aliyekuwa katika hedhi kabla ya kuchomoza Alfajiri hata kwa dakika moja, lakini akapata yakini kuwa ametwaharika, ikiwa ni katika Ramadhani basi atalazimika kufunga, na inakuwa funga yake siku hiyo ni sahihi, na wala halazimiki kuilipa siku hiyo, kwa sababu amefunga akiwa ametwaharika, hata kama hakuoga josho kubwa ila baada ya Alfajiri basi hakuna tatizo.

Kama vile Mwanaume akiwa katika janaba lililotokana na tendo la ndoa au kujiotea, na akala daku na wala hakuoga janaba ila baada ya Alfajiri, funga yake itakuwa sahihi.

Kwa mujibu wa hili, napenda kutoa angalizo la jambo lingine kwa wanawake, pindi mwanamke atakapo ijiwa na hedhi, na alikuwa kafunga siku hiyo, baadhi ya wanawake hudhania kwamba hedhi itakapowajia baada ya kufungua kabla ya kuswali swala ya Ishaa funga yao ya siku hiyo inakuwa imeharibika,

jambo hilo halina dalili katika sheria, bali hedhi itakapomuijia mwanamke baada ya Magharibi walau kwa muda mchache basi funga yake inakuwa imetimia na ni sahihi.

ﺟ2: إذا طهرت الحائض قبل طلوع الفجر ولو بدقيقةٍ واحدةٍ، ولكن تيقنت الطّهر، فإنه إذا كان في رمضان فإنه يلزمها الصوم، ويكون صومها ذلك اليوم صحيحًا، ولا يلزمها قضاؤه؛ لأنها صامت وهي طاهرٌ، وإن لم تغتسل إلا بعد طلوع الفجر فلا حرج،

كما أن الرجل لو كان جنبًا من جماعٍ أو احتلامٍ، وتسحر، ولم يغتسل إلا بعد طلوع الفجر، كان صومه صحيحًا.

وبهذه المناسبة أودّ أن أنبّه إلى أمرٍ آخر عند النّساء إذا أتاها الحيض وهي قد صامت ذلك اليوم، فإن بعض النّساء تظنّ أن الحيض إذا أتاها بعد فطرها قبل أن تصلّي العشاء فسد صوم ذلك اليوم،

وهذا لا أصل له، بل إن الحيض إذا أتاها بعد الغروب ولو بلحظةٍ فإن صومها تامٌّ وصحيحٌ.