Skip to content
Orodha ya Sura /

المُرسَلات

المُرسَلات is chapter 77 of the Quran and has 50 verses. This page presents it in full in the Uthmani script, with a verse-by-verse translation of its meaning.

50 Aya Sura Na. 77
Nenda kwenye aya
Kiswahili · Barawani
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

وَٱلۡمُرۡسَلَٰتِ عُرۡفٗا

Naapa kwa zinazo tumwa kwa upole!

Explanation & meanings · 1
  1. Naapa kwa Aya zilizo tumwa kwa ulimi wa Jibrili kumpelekea Muhammad kwa upole wa kawaida na kheri,

فَٱلۡعَٰصِفَٰتِ عَصۡفٗا

Na zinazo vuma kwa kasi!

Explanation & meanings · 1
  1. Na kwa Aya zenye kuzitwaa kwa nguvu dini nyengine zote za uwongo zikizipeperushia mbali,

وَٱلنَّٰشِرَٰتِ نَشۡرٗا

Na zikaeneza maeneo yote!

Explanation & meanings · 1
  1. Na kwa Aya zenye kueneza hikima na uwongofu katika nyoyo za walimwengu kwa uenezi mkubwa mno,

فَٱلۡفَٰرِقَٰتِ فَرۡقٗا

Na zinazo farikisha zikatawanya!

Explanation & meanings · 1
  1. Na zenye kufarikisha baina ya kweli na uwongo kwa mfarakano ulio wazi kabisa,

فَٱلۡمُلۡقِيَٰتِ ذِكۡرًا

Na zinazo peleka mawaidha!

Explanation & meanings · 1
  1. Na zenye kuwapa watu mawaidha ya kuwanufaisha,