Skip to content
Orodha ya Sura /

النَّبَإ

النَّبَإ is chapter 78 of the Quran and has 40 verses. This page presents it in full in the Uthmani script, with a verse-by-verse translation of its meaning.

40 Aya Sura Na. 78
Nenda kwenye aya
Kiswahili · Barawani
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

عَمَّ يَتَسَآءَلُونَ

WANAULIZANA nini?

Explanation & meanings · 1
  1. Wanaulizana nini hao makafiri?

عَنِ ٱلنَّبَإِ ٱلۡعَظِيمِ

Ile khabari kuu!

Explanation & meanings · 1
  1. Wanaulizana khabari kubwa, khabari ya kufufuliwa,

ٱلَّذِي هُمۡ فِيهِ مُخۡتَلِفُونَ

Ambayo kwayo wanakhitalifiana.

Explanation & meanings · 1
  1. Ambayo wao wamezama ndani yake kukhitalifiana baina ya wenye kuikataa na wenye kuitilia shaka.

كَلَّا سَيَعۡلَمُونَ

La! Karibu watakuja jua.

Explanation & meanings · 1
  1. Kuwazuia kuulizana huko wanaambiwa kuwa watakuja ujua ukweli wa mambo hapo watapo ona kufufuliwa kumetokea khasa.

ثُمَّ كَلَّا سَيَعۡلَمُونَ

Tena la! Karibu watakuja jua.

Explanation & meanings · 1
  1. Tena kuwazuia, watakuja jua itapo wateremkia adhabu.