Kila wema ni sadaka
Imepokelewa kutoka kwa Jaabir -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- kuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema:
"Kila wema ni sadaka"
«كُلُّ مَعْرُوفٍ صَدَقَةٌ».
Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa kila wema na kuwanufaisha wengine kuanzia kauli au matendo huwa ni sadaka, na kuna malipo na thawabu.
معروف : المعروف اسم جامع لكل ما فيه نفع للآخرين من قول أو فعل.
Nikuwa sadaka haishii tu katika vile anavyovitoa mtu katika mali yake, bali inajumuisha kila kheri anayoifanya mwanadamu au kuitamka na kuifikisha kwa wengine.
Hapa kuna himizo la kutenda wema, na kila jambo lenye manufaa kwa wengine.
Kutodharau kitu katika wema, hata kama ni kidogo.
Swahiih Al Bukhaariy (8/ 11) (6021).
Swahiih Muslim (2/ 697) (1005).
Zaidi (4)
منحة العلام في شرح بلوغ المرام.
لعبد الله الفوزان (10/ 117).
توضيح الأحكام من بلوغ المرام.
للبسام (7/ 341).