Skip to content
Orodha ya Sura /

Al-Ghashiyah

ﰅ

Al-Ghashiyah is chapter 88 of the Quran and has 26 verses. This page presents it in full in the Uthmani script, with a verse-by-verse translation of its meaning.

26 Aya Sura Na. 88
Nenda kwenye aya
Kiswahili · Barawani
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

هَلۡ أَتَىٰكَ حَدِيثُ ٱلۡغَٰشِيَةِ

Je! Imekufikia khabari ya msiba wa kufudikiza?

Explanation & meanings · 1
  1. Je! Ewe Muhammad! Imepata kukujia hadithi ya Kiyama ambacho kwa vitisho vyake kitawafanya watu wazimie?

وُجُوهٞ يَوۡمَئِذٍ خَٰشِعَةٌ

Siku hiyo nyuso zitainama!

Explanation & meanings · 1
  1. Siku hiyo ya Kiyama zitakuwepo nyuso zimedhalilika,

عَامِلَةٞ نَّاصِبَةٞ

Zikifanya kazi, nazo taabani.

Explanation & meanings · 1
  1. Zimechoka, taabani kwa shughuli na mashaka ya Motoni,

تَصۡلَىٰ نَارًا حَامِيَةٗ

Ziingie katika Moto unao waka .

Explanation & meanings · 1
  1. Zinaingia kwenye Moto unao waka kwa nguvu!

تُسۡقَىٰ مِنۡ عَيۡنٍ ءَانِيَةٖ

Zikinyweshwa kutoka chemchem inayo chemka.

Explanation & meanings · 1
  1. Wananywesha maji yanayo toka kwenye chemchem inayo tokota.