Skip to content
Orodha ya Sura /

الأعلى

الأعلى is chapter 87 of the Quran and has 19 verses. This page presents it in full in the Uthmani script, with a verse-by-verse translation of its meaning.

19 Aya Sura Na. 87
Nenda kwenye aya
Kiswahili · Barawani
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

سَبِّحِ ٱسۡمَ رَبِّكَ ٱلۡأَعۡلَى

Litakase jina la Mola wako Mlezi aliye juu kabisa!

Explanation & meanings · 1
  1. Litakase jina la Mola wako Mlezi lilio tukufu na kila kitu kisicho kuwa kinaelekeana nalo.

ٱلَّذِي خَلَقَ فَسَوَّىٰ

Aliye umba, na akaweka sawa!

Explanation & meanings · 1
  1. Aliye umba kila kitu, na akajaalia uumbaji wote sawa sawa katika hukumu na kupangana.

وَٱلَّذِي قَدَّرَ فَهَدَىٰ

Na ambaye amekadiria na akaongoa,.

Explanation & meanings · 1
  1. Na akakadiria kwa kila kitu kwa mujibu wa maslaha yake, na akakiongoza.

وَٱلَّذِيٓ أَخۡرَجَ ٱلۡمَرۡعَىٰ

Na aliye otesha malisho!

Explanation & meanings · 1
  1. Na ambaye akatoa kwenye ardhi mimea namna mbali mbali ya kuwalisha wanyama.

فَجَعَلَهُۥ غُثَآءً أَحۡوَىٰ

Kisha akayafanya makavu, meusi.

Explanation & meanings · 1
  1. Na akaifanya mimea hiyo baada ya kuwa kijani imestawi, ikakauka na imekuwa myeusi!