Skip to content
Orodha ya Sura /

الفَجر

الفَجر is chapter 89 of the Quran and has 30 verses. This page presents it in full in the Uthmani script, with a verse-by-verse translation of its meaning.

30 Aya Sura Na. 89
Nenda kwenye aya
Kiswahili · Barawani
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

وَٱلۡفَجۡرِ

Naapa kwa alfajiri!

Explanation & meanings · 1
  1. Naapa kwa mwangaza wa asubuhi unapo ufukuza usiku.

وَلَيَالٍ عَشۡرٖ

Na kwa masiku kumi!

Explanation & meanings · 1
  1. Na kwa masiku kumi yaliyo tukuzwa na Mwenyezi Mungu. (Na hayo ni masiku kumi ya mwanzo wa Mwezi wa Alhaj, Mfungo Tatu).

وَٱلشَّفۡعِ وَٱلۡوَتۡرِ

Na kwa viwili viwili na kimoja kimoja!

Explanation & meanings · 1
  1. Na shafi' yaani hisabu inayo gawika kwa mbili, kama 4, 6, 8 n.k. na witri, yaani isiyo gawika kwa mbili, kama 1, 3, 5 n.k. katika kila kitu.

وَٱلَّيۡلِ إِذَا يَسۡرِ

Na kwa usiku unapo pita!

Explanation & meanings · 1
  1. Na kwa usiku unapo pita kwa kwenda ulimwengu kwa namna ya ajabu.

هَلۡ فِي ذَٰلِكَ قَسَمٞ لِّذِي حِجۡرٍ

Je! Hapana katika haya kiapo kwa mwenye akili?

Explanation & meanings · 1
  1. Je! Katika vitu vilivyo tajwa vinavyo onekana kwa akili hapana kiapo cha kukinaisha?