Skip to content
Orodha ya Sura /

الطَّارق

الطَّارق is chapter 86 of the Quran and has 17 verses. This page presents it in full in the Uthmani script, with a verse-by-verse translation of its meaning.

17 Aya Sura Na. 86
Nenda kwenye aya
Kiswahili · Barawani
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

وَٱلسَّمَآءِ وَٱلطَّارِقِ

Naapa kwa mbingu na Kinacho kuja usiku!

Explanation & meanings · 1
  1. Naapa kwa mbingu na nyota inayo tokeza usiku!

وَمَآ أَدۡرَىٰكَ مَا ٱلطَّارِقُ

Na nini kitakacho kujuulisha ni nini hicho Kinacho kuja usiku?

Explanation & meanings · 1
  1. Na kitu gani kitakujuvya ukweli wa nyota hii? Ni hiyo inayotoa mwanga wake katika giza.

ٱلنَّجۡمُ ٱلثَّاقِبُ

Ni Nyota yenye mwanga mkali.

Explanation & meanings · 1
  1. Na kitu gani kitakujuvya ukweli wa nyota hii? Ni hiyo inayotoa mwanga wake katika giza.

إِن كُلُّ نَفۡسٖ لَّمَّا عَلَيۡهَا حَافِظٞ

Hapana nafsi ila inayo mwangalizi.

Explanation & meanings · 1
  1. Hapana nafsi ila inayo mlinzi wa kuiangalia na kudhibiti vitendo vyake.

فَلۡيَنظُرِ ٱلۡإِنسَٰنُ مِمَّ خُلِقَ

Hebu naajitazame mwanaadamu ameumbwa kwa kitu gani?

Explanation & meanings · 1
  1. Basi naafikiri mtu, yeye kaumbwa kutokana na nini?