Skip to content
Orodha ya Sura /

القَلَم

القَلَم is chapter 68 of the Quran and has 52 verses. This page presents it in full in the Uthmani script, with a verse-by-verse translation of its meaning.

52 Aya Sura Na. 68
Nenda kwenye aya
Kiswahili · Barawani
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

نٓۚ وَٱلۡقَلَمِ وَمَا يَسۡطُرُونَ

Nuun. Naapa kwa kalamu na yale wayaandikayo!

Explanation & meanings · 1
  1. Nuun, ndio harufi ya N, iliyo anzia Sura hii ni kama kupinzana na hao wanao kadhibisha, na ili kuwazindua wenye kusadiki. Naapa kwa kalamu wanayo andikia Malaika na wenginewe, na hayo mambo ya kheri na manufaa wanayo yaandika,

مَآ أَنتَ بِنِعۡمَةِ رَبِّكَ بِمَجۡنُونٖ

Kwa neema ya Mola wako Mlezi wewe si mwendawazimu.

Explanation & meanings · 1
  1. Hakika wewe, na Mwenyezi Mungu amekuneemesha kwa kukupa Unabii, si mchachefu wa akili, wala mpumbavu wa mawazo.

وَإِنَّ لَكَ لَأَجۡرًا غَيۡرَ مَمۡنُونٖ

Na kwa hakika wewe una malipo yasiyo katika.

Explanation & meanings · 1
  1. Na hakika unapata thawabu kubwa zisio katika kwa ajili ya kufikisha Ujumbe.

وَإِنَّكَ لَعَلَىٰ خُلُقٍ عَظِيمٖ

Na hakika wewe una tabia tukufu.

Explanation & meanings · 1
  1. Na hakika wewe bila ya shaka umeshikamana na sifa nzuri kabisa na vitendo vizuri kabisa alivyo kuumba navyo Mwenyezi Mungu.

فَسَتُبۡصِرُ وَيُبۡصِرُونَ

Karibu utaona, na wao wataona!

Explanation & meanings · 1
  1. Karibuni hivi, ewe Muhammad, utaona, na makafiri wataona,