Skip to content

Ni ipi hukumu ya mwanamke kafikiwa na mzunguko wa hedhi baada ya kuingia wakati wa swala, je inawajibika kwake yeye kulipa akitwaharika? Na hivyo hivyo pindi akitwaharika kabla ya kutoka muda wa swala?

السؤال

Swali la 1:

Ni ipi hukumu ya mwanamke kafikiwa na mzunguko wa hedhi baada ya kuingia wakati wa swala, je inawajibika kwake yeye kulipa akitwaharika? Na hivyo hivyo pindi akitwaharika kabla ya kutoka muda wa swala?

س31: ما الحكم إذا حاضت المرأة بعد دخول وقت الصلاة؟ وهل يجب عليها أن تقضيها إذا طهرت؟ وكذلك إذا طهرت قبل خروج وقت الصلاة؟

الجواب

Jawabu la 1:

Kwanza: Mwanamke akiingia katika mzunguko wa damu ya hedhi baada ya kuingia wakati wa swala basi inawajibika kwake akitwaharika alipe swala ambazo alipatwa na mzunguko katika wakati wake, ikiwa hajaswali kabla ya kuingiwa na hedhi.

Na hili ni kwa mujibu wa kauli yake Mtume rehema na amani za Allah zimfikie:

"Atakaye idiriki rakaa katika swala basi amediriki swala"

Ikiwa mwanamke ataupata muda wa swala kiasi cha rakaa moja, kisha akaingia katika hedhi kabla hajaswali, itamlazimu kukidhi (kulipa) swala hiyo pindi atakapo twaharika.

Pili: Ikiwa mwanamke atatwaharika kutokana na hedhi kabla muda wa swala haujatoka, basi itamuwajibikia kulipa swala hiyo. Na lau atatwaharika kabla ya jua kuchomoza kwa kiasi cha rakaa moja itamuwajibikia kulipa swala ya Alfajiri,

na lau atatwaharika kabla ya jua kuzama kwa kiasi cha rakaa moja itamuwajibikia kuswali swala ya Alasiri,

na lau atatwaharika kabla ya usiku kufikia katikati itamuwajibikia kulipa swala ya Ishaa,

na ikiwa atatwaharika baada ya nusu ya usiku, haitamuwajibikia swala ya Ishaa,

Allah Mtukufu anasema: "...Na mtakapopata amani mkawa katika salama, hapana vita, basi simamisheni swala, kwa hakika swala kwa waumini ni faradhi iliyopangiwa wakati maalumu" [Annisai: 103],

Yaani: Ni faradhi iliyopangiwa wakati maalumu, haifai kwa mtu kuitoa swala nje ya wakati wake (akaswali baada ya kutoka muda wake), wala kuiswali kabla ya kuingia wakati wake.

ﺟ31: أولًا: المرأة إذا حاضت بعد دخول الوقت -أي: بعد دخول وقت الصلاة- فإنه يجب عليها إذا طهرت أن تقضي تلك الصلاة الّتي حاضت في وقتها، إذا لم تصلّها قبل أن يأتيها الحيض،

وذلك لقول الرسول ﷺ:

«مَنْ أَدْرَكَ رَكْعَةً مِنَ الصَّلَاةِ فَقَدْ أَدْرَكَ الصَّلَاةَ» [1]،

فإذا أدركت المرأة من وقت الصلاة مقدار ركعةٍ، ثم حاضت قبل أن تصلّي، فإنها إذا طهرت يلزمها القضاء.

[11] تقدم تخريجه.

ثانيًا: إذا طهرت من الحيض قبل خروج وقت الصلاة فإنه يجب عليها قضاء تلك الصلاة، فلو طهرت قبل أن تطلع الشمس بمقدار ركعةٍ وجب عليها قضاء صلاة الفجر،

ولو طهرت قبل غروب الشمس بمقدار ركعةٍ وجبت عليها صلاة العصر،

ولو طهرت قبل منتصف الليل بمقدار ركعةٍ وجب عليها قضاء صلاة العشاء،

فإن طهرت بعد منتصف الليل لم يجب عليها صلاة العشاء، وعليها أن تصلّي الفجر إذا جاء وقتها، قال الله سبحانه وتعالى:

﴿...فَإِذَا ٱطۡمَأۡنَنتُمۡ فَأَقِيمُواْ ٱلصَّلَوٰةَۚ إِنَّ ٱلصَّلَوٰةَ كَانَتۡ عَلَى ٱلۡمُؤۡمِنِينَ كِتَٰبٗا مَّوۡقُوتٗا﴾

[النساء:103]،

أي: فرضًا مؤقتًا بوقتٍ محدودٍ، لا يجوز للإنسان أن يخرج الصلاة عن وقتها، ولا أن يبدأ بها قبل وقتها.