Skip to content
Orodha ya Sura /

النَّازعَات

النَّازعَات is chapter 79 of the Quran and has 46 verses. This page presents it in full in the Uthmani script, with a verse-by-verse translation of its meaning.

46 Aya Sura Na. 79
Nenda kwenye aya
Kiswahili · Barawani
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

وَٱلنَّٰزِعَٰتِ غَرۡقٗا

Naapa kwa wanao komoa kwa nguvu!

Explanation & meanings · 1
  1. Ninaapa kwa kila kilicho pewa uwezo wa kuving'oa vitu kutokana na pahala pao kwa nguvu,

وَٱلنَّٰشِطَٰتِ نَشۡطٗا

Na kwa wanao toa kwa upole!

Explanation & meanings · 1
  1. Na kwa kila kilicho pewa uwezo wa kuvitoa vitu kwa utaratibu na ulaini,

وَٱلسَّٰبِحَٰتِ سَبۡحٗا

Na wanao ogelea!

Explanation & meanings · 1
  1. Na kwa kila kilicho pewa mbio za kutekeleza kazi yake kwa sahala na wepesi.

فَٱلسَّٰبِقَٰتِ سَبۡقٗا

Wakishindana mbio!

Explanation & meanings · 1
  1. Na kwa vinavyo shindania kutimiza waajibu ulio twikwa juu yao kushindania kwa juhudi,

فَٱلۡمُدَبِّرَٰتِ أَمۡرٗا

Wakidabiri mambo.

Explanation & meanings · 1
  1. Na vinavyo dabiri, kupanga, mambo na kuyaendesha kwa mujibu wa vilivyo khusishwa,