Skip to content

Akitwaharika mwenye hedhi au nifasi muda wa Alasiri, je analazimika kuswali swala ya Adhuhuri na Alasiri, au halazimiki kuswali isipokuwa Alasiri peke yake?

السؤال

Swali la 1:

Akitwaharika mwenye hedhi au nifasi muda wa Alasiri, je analazimika kuswali swala ya Adhuhuri na Alasiri, au halazimiki kuswali isipokuwa Alasiri peke yake?

س12: إذا طهرت الحائض أو النّفساء وقت العصر، فهل تلزمها صلاة الظّهر مع العصر، أو لا يلزمها سوى العصر فقط؟

الجواب

Jawabu la 1:

Kauli yenye kutegemewa katika swala hili nikuwa: Analazimika kuswali swala ya Alasiri pekee kwa sababu hakuna dalili juu ya ulazima kwake kuswali Adhuhuri, na asili ni kutokuwa na dhima ya jambo na Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema:

"Atakayeupata wakati wa swala ya Alasiri kwa kiwango cha rakaa moja kabla jua halijazama basi ameipata Lasiri",

Na hakutaja kwamba amediriki Adhuhuri, ingekuwa swala ya Adhuhuri ni lazima kwa mtu huyu basi angebainisha Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- na mwanamke akitokwa na damu ya hedhi, baada ya kuingia wakati wa Adhuhuri basi haimlazimu akitwaharika kulipa isipokuwa swala ya Adhuhuri pekee na hatolipa Alasiri pamoja na kwamba swala ya Adhuhuri hujumuishwa na swala ya Alasiri na wala hakuna tofauti kati yake na sura iliyoulizwa katika swali.

Na kuhusu suala hili, kauli ya kutegemewa nikwamba halazimiki isipokuwa swala ya Alasiri pekee kutokana na dalili ya kisheria na kiyasi (Kuoanisha mambo), na hivyo hivyo ikiwa ametwaharika kabla ya kutoka wakati wa swala ya Ishaa, basi halazimiki isipokuwa kuswali swala ya Ishaa peke yake, wala halazimiki kuswali swala ya Magharibi.

ﺟ12: القول الراجح في هذه المسألة: أنه لا يلزمها إلا العصر فقط؛ لأنه لا دليل على وجوب صلاة الظّهر، والأصل براءة الذّمة، ثم إن النبي ﷺ قال:

«مَنْ أَدْرَكَ رَكْعَةً مِنَ الْعَصْرِ قَبْلَ أَنْ تَغْرُبَ الشَّمْسُ فَقَدْ أَدْرَكَ الْعَصْرَ» [1]،

ولم يذكر أنه أدرك الظّهر، ولو كان الظّهر واجبًا لبينه النبيّ ﷺ، ولأن المرأة لو حاضت بعد دخول وقت الظّهر لم يلزمها إلا قضاء صلاة الظّهر دون صلاة العصر، مع أن الظّهر تجمع إلى العصر، ولا فرق بينها وبين الصّورة التي وقع السّؤال عنها.

[2] البخاري، كتاب الصوم، باب الحائض تترك الصوم والصلاة (1951).

وعلى هذا يكون القول الراجح أنه لا يلزمها إلا صلاة العصر فقط؛ لدلالة النصّ والقياس عليها، وكذلك الشأن فيما لو طهرت قبل خروج وقت العشاء، فإنه لا يلزمها إلا صلاة العشاء، ولا تلزمها صلاة المغرب.