Skip to content

Mwanamke mjamzito akitokwa na damu mchana wa Ramadhani, je jambo hili lita athiri swaumu yake?

السؤال

Swali la 1:

Mwanamke mjamzito akitokwa na damu mchana wa Ramadhani, je jambo hili lita athiri swaumu yake?

س14: نزول الدم من الحامل في نهار رمضان، هل يؤثّر على صومها؟

الجواب

Jawabu la 1:

Itakapotoka damu ya hedhi na mwanamke akiwa amefunga basi funga yake itaharibika, kutokana na kauli ya Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-:

"Hivi haikuwa wakati alipokuwa katika mzunguko wake wa hedhi haswali wala hafungi?"

Na kwa ajili hii tunazingatia hili ni katika mambo yanayofunguza swaumu, na damu ya uzazi ni mfano wake, na kutoka damu ya hedhi na nifasi vinaharibu funga ya mtu.

Na mwanamke mjamzito akitokwa na damu mchana wa Ramadhani basi ikiwa ni hedhi basi hiyo ni hedhi kama ilivyo hedhi ya mwanamke asiye mjamzito, na inaathiri swaumu yake, na ikiwa siyo hedhi basi haiathiri funga yake.

Na damu ya hedhi ambayo inaweza mtokea mwanamke mwenye mimba ni damu ya hedhi ambayo haikatiki kwake tangu kubeba ujauzito huo, bali inamjia katika zile nyakati zake alizozizoea kuwa damu ya hedhi humuijia, basi hedhi hii kwa kauli yenye kutegemewa inathibiti kwake na inachukua hukumu za hedhi ya kawaida.

Ama ikikatika damu hiyo ya hedhi naye bado mjamzito, kisha ikawa baada ya hapo anaona damu katika wakati ambao siyo wa mzunguko wake wa kisheria, hili haliathiri funga yake, kwa sababu hii si hedhi.

ﺟ14: إذا خرج دم الحيض والأنثى صائمةٌ فإن صومها يفسد؛ لقول النبيّ ﷺ:

«أَلَيْسَ إِذَا حَاضَتْ لَمْ تُصَلِّ، وَلَمْ تَصُمْ؟» [1]

ولهذا نعدّه من المفطّرات، والنّفاس مثله، وخروج دم الحيض والنّفاس مفسدٌ للصوم.

[3] البخاري، كتاب الصوم، باب الحائض تترك الصوم والصلاة (1951).

ونزول الدم من الحامل في نهار رمضان إذا كان حيضًا فإنه كحيض غير الحامل، أي: يؤثّر على صومها، وإن لم يكن حيضًا فإنه لا يؤثّر.

والحيض الّذي يمكن أن يقع من الحامل هو أن يكون حيضًا مطردًا لم ينقطع عنها منذ حملت، بل كان يأتيها في أوقاتها المعتادة، فهذا حيضٌ على القول الراجح، يثبت له أحكام الحيض.

أما إذا انقطع الدم عنها، ثم صارت بعد ذلك ترى دمًا ليس هو الدم المعتاد، فإن هذا لا يؤثّر على صيامها؛ لأنه ليس بحيضٍ.