Skip to content
Orodha ya Sura /

اللَّيل

اللَّيل is chapter 92 of the Quran and has 21 verses. This page presents it in full in the Uthmani script, with a verse-by-verse translation of its meaning.

21 Aya Sura Na. 92
Nenda kwenye aya
Kiswahili · Barawani
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

وَٱلَّيۡلِ إِذَا يَغۡشَىٰ

Naapa kwa usiku unapo funika!

Explanation & meanings · 1
  1. Naapa kwa usiku kinapo enea kiza chake!

وَٱلنَّهَارِ إِذَا تَجَلَّىٰ

Na mchana unapo dhihiri!

Explanation & meanings · 1
  1. Na naapa kwa mchana unapo zagaa mwangaza wake!

وَمَا خَلَقَ ٱلذَّكَرَ وَٱلۡأُنثَىٰٓ

Na kwa Aliye umba dume na jike!

Explanation & meanings · 1
  1. Na naapa kwa Mjuzi aliye umba viwili viwili, dume na jike, katika kila vinavyo zaliwa!

إِنَّ سَعۡيَكُمۡ لَشَتَّىٰ

Hakika juhudi zenu bila ya shaka ni mbali mbali.

Explanation & meanings · 1
  1. Hakika juhudi zenu bila ya shaka zimekhitalifiana; kwani wapo wenye kubahatika katika juhudi zao, na wako wasio bahatika.

فَأَمَّا مَنۡ أَعۡطَىٰ وَٱتَّقَىٰ

Ama mwenye kutoa na akamchamngu!

Explanation & meanings · 1
  1. Ama mwenye kutoa katika Njia ya Mwenyezi Mungu, na akamkhofu Mola wake Mlezi, na kwa hivyo akaepuka anayo yakataza,