Skip to content
Orodha ya Sura /

الضُّحى

الضُّحى is chapter 93 of the Quran and has 11 verses. This page presents it in full in the Uthmani script, with a verse-by-verse translation of its meaning.

11 Aya Sura Na. 93
Nenda kwenye aya
Kiswahili · Barawani
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

وَٱلضُّحَىٰ

Naapa kwa mchana!

Explanation & meanings · 1
  1. Naapa kwa wakati wa kupanda juu jua, na ni wakati wa uchangamfu na kazi!

وَٱلَّيۡلِ إِذَا سَجَىٰ

Na kwa usiku unapo tanda!

Explanation & meanings · 1
  1. Na naapa kwa usiku unapo tulia na ukatanda kote kiza chake!

مَا وَدَّعَكَ رَبُّكَ وَمَا قَلَىٰ

Mola wako Mlezi hakukuacha, wala hakukasirika nawe.

Explanation & meanings · 1
  1. Ewe Muhammad! Mola wako Mlezi hakukuacha, wala hakukuchukia.

وَلَلۡأٓخِرَةُ خَيۡرٞ لَّكَ مِنَ ٱلۡأُولَىٰ

Na bila ya shaka wakati ujao utakuwa bora kwako kuliko ulio tangulia.

Explanation & meanings · 1
  1. Na matokeo ya mambo yako, mwisho wake, yatakuwa bora kuliko mwanzo wake.

وَلَسَوۡفَ يُعۡطِيكَ رَبُّكَ فَتَرۡضَىٰٓ

Na Mola wako Mlezi atakupa mpaka uridhike.

Explanation & meanings · 1
  1. Na ninaapa kuwa bila ya shaka hapo Mola wako Mlezi atakupa kheri za duniani na Akhera hata utaridhia.