Skip to content
Orodha ya Sura /

الانفِطَار

ﯿ

الانفِطَار is chapter 82 of the Quran and has 19 verses. This page presents it in full in the Uthmani script, with a verse-by-verse translation of its meaning.

19 Aya Sura Na. 82
Nenda kwenye aya
Kiswahili · Barawani
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

إِذَا ٱلسَّمَآءُ ٱنفَطَرَتۡ

Mbingu itapo chanika!

Explanation & meanings · 1
  1. Itakapo pasuka mbingu,

وَإِذَا ٱلۡكَوَاكِبُ ٱنتَثَرَتۡ

Na nyota zitapo tawanyika!

Explanation & meanings · 1
  1. Na nyota zitakapo pukutika na kutawanyika,

وَإِذَا ٱلۡبِحَارُ فُجِّرَتۡ

Na bahari zitakapo pasuliwa!

Explanation & meanings · 1
  1. Na bahari zikafurika na kuingiliana kwa kuondoka viziwizi baina yao,

وَإِذَا ٱلۡقُبُورُ بُعۡثِرَتۡ

Na makaburi yatapo fukuliwa!

Explanation & meanings · 1
  1. Na makaburi yakafunuliwa na wakatoka maiti walio kuwamo,

عَلِمَتۡ نَفۡسٞ مَّا قَدَّمَتۡ وَأَخَّرَتۡ

Hapo kila nafsi itajua ilicho tanguliza, na ilicho bakisha nyuma.

Explanation & meanings · 1
  1. Hapo basi kila nafsi itajua nini kheri au shari iliyo tanguliza na iliyo chelewesha.