Mwanamke mwenye hedhi au nifasi akitwaharika kabla ya Alfajiri, je swaumu yake iko sahihi au la?
السؤال
Swali la 1:
Mwanamke mwenye hedhi au nifasi akitwaharika kabla ya Alfajiri, je swaumu yake iko sahihi au la?
س7: إذا طهرت الحائض أو النّفساء قبل الفجر، ولم تغتسل إلا بعد الفجر، فهل يصحّ صومها، أو لا؟
الجواب
Jawabu la 1:
Naam, iko sahihi swaumu ya mwanamke mwenye hedhi atakapotwaharika kabla ya Alfajiri, na hakuoga josho kubwa la kujitwaharisha isipokuwa baada ya Alfajiri, na hukumu hii ni pamoja na wanawake walio katika nifasi, kwa sababu kwa wakati huo ni katika watu wanaotakiwa kufunga, na huu ni mfano wa aliyepatwa na janaba, na ikachomoza Alfajiri akiwa na janaba, swaumu yake ni sahihi;
Kutokana na kauli yake Allah -Mtukufu-: "Na sasa hivi waingilieni na tafuteni yale aliyowaandikieni Allah kwa ajili yenu, na kuleni na kunyweni mpaka ubainike kwenu nyinyi weupe wa Alfajiri ya kweli itokanayo na giza la usiku" (Al baqara: 187)
Na akiruhusu Allah kumuingilia mwanamke mpaka ibainike Alfajiri ya kweli basi inamlazimu katika hilo kusiwe na kuoga josho kubwa isipokuwa baada ya kuchomoza Alfajiri, kutokana na hadithi ya Aisha -radhi za Allah ziwe juu yake- kwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- alikuwa akiamka asubuhi akiwa na janaba kutokana na kumuingilia mkewe naye akiwa katika swaumu.
Yaani: Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- alikuwa haogi janaba isipokuwa baada ya kuchomoza Alfajiri.
ﺟ7: نعم، يصحّ صوم المرأة الحائض إذا طهرت قبل الفجر، ولم تغتسل إلا بعد طلوع الفجر، وكذلك النّفساء؛ لأنها حينئذٍ من أهل الصوم، وهي شبيهةٌ بمن عليه جنابةٌ، إذا طلع الفجر وهو جنبٌ فإن صومه يصحّ؛ لقوله تعالى:
﴿...فَٱلۡـَٰٔنَ بَٰشِرُوهُنَّ وَٱبۡتَغُواْ مَا كَتَبَ ٱللَّهُ لَكُمۡۚ وَكُلُواْ وَٱشۡرَبُواْ حَتَّىٰ يَتَبَيَّنَ لَكُمُ ٱلۡخَيۡطُ ٱلۡأَبۡيَضُ مِنَ ٱلۡخَيۡطِ ٱلۡأَسۡوَدِ مِنَ ٱلۡفَجۡرِ...﴾
[البقرة:187]،
وإذا أذن الله تعالى بالجماع إلى أن يتبين الفجر لزم من ذلك ألّا يكون الاغتسال إلا بعد طلوع الفجر، ولحديث عائشة رضي الله عنها
«أَنَّ النَّبِيَّ ﷺ كَانَ يُصْبِحُ جُنُبًا مِنْ جِمَاعِ أَهْلِهِ وَهُوَ صَائِمٌ» [1].
أي: أنه عليه الصلاة والسلام لا يغتسل عن الجنابة إلا بعد طلوع الصّبح.
[1] البخاري، كتاب الصوم، باب اغتسال الصائم (1931)، ومسلم، كتاب الصوم، باب صحة صوم من طلع عليه الفجر وهو جنب (75) (1109).