Skip to content

Ikiwa mzunguko wa mwezi wa mwanamke ni siku nane au siku saba, kisha mzunguko wake ukaendelea mara moja au mara nyingine zaidi ya siku hizo, ni ipi hukumu yake?

السؤال

Swali la 1:

Ikiwa mzunguko wa mwezi wa mwanamke ni siku nane au siku saba, kisha mzunguko wake ukaendelea mara moja au mara nyingine zaidi ya siku hizo, ni ipi hukumu yake?

س4: إذا كانت المرأة عادتها الشهرية ثمانية أيامٍ أو سبعة أيامٍ، ثم استمرت معها مرةً أو مرتين أكثر من ذلك، فما الحكم؟

الجواب

Jawabu la 1:

Ikiwa mzunguko wa mwanamke huyu ni siku sita au saba, kisha muda wa kuwa na damu ukarefuka, ukawa siku nane, au saba, au kumi, au kumi na moja, basi hatoswali mwanamke huyu mpaka atwaharike,

Na hilo ni kwa sababu Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- hakuweka ukomo maalumu wa siku za mzunguko wa hedhi.

Na amesema Allah Mtukufu: "Na wanakuuliza kuhusu hedhi, sema: Huo ni uchafu" [Al-baqara: 222],

Muda wowote damu hii ikiwepo basi mwanamke atabaki katika hali hiyo mpaka atwaharike, na aoge josho kubwa, kisha aswali, na ukija mwezi wa pili siku zimepungua ukilinganisha na mwezi wa kwanza, basi akitwaharika ataoga hata kama mwezi huu haukuwa kama ule uliopita.

Na jambo la msingi nikuwa; Muda wowote mwanamke akiwa katika mzunguko wa hedhi basi hatoswali, uwe mzunguko huo una siku kama mzunguko uliopita, au zimezidi au zimepungua, atakapotwaharika ataswali.

ﺟ4: إذا كانت عادة هذه المرأة ستة أيامٍ أو سبعةً، ثم طالت هذه المدة، وصارت ثمانيةً أو تسعةً أو عشرةً أو أحد عشر يومًا فإنها تبقى لا تصلّي حتى تطهر،

وذلك لأن النبي ﷺ لم يحد حدًّا معيّنًا في الحيض، وقد قال الله تعالى:

﴿وَيَسۡـَٔلُونَكَ عَنِ ٱلۡمَحِيضِۖ قُلۡ هُوَ أَذٗى...﴾

[البقرة:222]،

فمتى كان هذا الدم باقيًا فإن المرأة على حالها حتى تطهر، وتغتسل، ثم تصلّي، فإذا جاءها في الشهر الثاني ناقصًا عن ذلك فإنها تغتسل إذا طهرت وإن لم يكن على المدة السابقة.

والمهمّ أن المرأة متى كان الحيض معها موجودًا فإنها لا تصلّي، سواءٌ كان الحيض موافقًا للعادة السابقة، أو زائدًا عنها، أو ناقصًا، وإذا طهرت تصلّي.