Nilimwendea Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- nikitaka kuwa muislamu, akaniamrisha nioge kwa maji na mkunazi
Kutoka kwa Kaisi bin Aswim -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema:
Nilimwendea Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- nikitaka kuwa muislamu, akaniamrisha nioge kwa maji na mkunazi.
أتيتُ النبيَّ صلى الله عليه وسلم أُريدُ الإسلامَ، فأَمَرَني أن أغتَسِلَ بماءٍ وسِدرٍ.
Alikuja Kaisi bin Aswim kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akitaka kusilimu, Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akamuamrisha aoge kwa maji na mti wa mkunazi; kwakuwa majani yake hutumika katika usafi; na kwakuwa yana harufu nzuri.
Sheria ya kafiri kuoga anapoingia katika Uislamu.
Thamani ya Uislamu na kutilia kwake umuhimu mwili na roho vyote kwa pamoja.
Maji kuchanganyika na vitu safi haviyatoa katika twahara yake.
Visimama badala ya mkunazi vifaa vya usafi vya kisasa, kama sabuni na mfano wake.
Sunanu Abii Daud (1/ 266) (355).
Sunanu Tirmidhiy (1/ 595) (605).
Sunanu Al Nasaai (1/ 109) (188).
Zaidi (3)
معالم السنن (1/111).
ذخيرة العقبى (4/131).
شرح سنن أبي داود للعباد (54/ 10).