عربي - Arabic English Qafár af - Afar Afrikaans - Afrikanns Akan Shqip - Albanian አማርኛ - Amharic Հայերեն - Armenian অসমীয়া - Assamese Azərbaycanca - Azerbaijani Bamanankan - Bambara Bassa Bemba বাংলা - Bengali Bosanski - Bosnian Български - Bulgarian မြန်မာဘာသာ - Burmese Bisaya - Cebuano Cham Нохчий - Chechen chiCheŵa - Chewa 中文 - Chinese Адыгэбзэ - Circassian Hrvatski - Croatian Česky - Czech Dagbani Dansk - Danish فارسی دری - Dari Dendi ދިވެހި ބަސް - Dhivehi Nederlands - Dutch إستوني - Estonian Suomi - Finnish Français - French Fulfulde - Fula ქართული - Georgian Deutsch - German Ελληνικά - Greek ગુજરાતી - Gujrati Kreyòl ayisyen - Haitian Creole Hausa हिन्दी - Hindi Magyar - Hungarian Igbo Indonesia - Indonesian Italiano - Italian 日本語 - Japanese Jóola - Jola ಕನ್ನಡ - Kannada Қазақша - Kazakh ភាសាខ្មែរ - Khmer Kikuyu Ikinyarwanda - Kinyarwanda Ikirundi - Kirundi 한국어 - Korean كوردی سۆرانی - kurdish كوردي kurmancî - Kurmanji Kyrgyz ລາວ - Lao latviešu - Latvian Lingala lietuvių - Lithuanian Luganda Македонски - Macedonian Maguindanaon Malagasy - Malagasy Bahasa Melayu - Malay മലയാളം - Malayalam Mandinka मराठी - Marathi Mõõré - Moore नेपाली - Nepali أنكو - NKo Norwegian ଓଡ଼ିଆ - Odia oromoo - Oromo پښتو - Pashto فارسی - Persian Polski - Polish Portuguese ਪੰਜਾਬੀ - Punjabi Română - Romanian Русский - Russian Српски - Serbian Shona සිංහල - Sinhala Slovenščina - Slovenian Soomaaliga - Somali Soninke Sesotho - Sotho Español - Spanish Kiswahili - Swahili Svenska - Swedish Tagalog Тоҷикӣ - Tajik தமிழ் - Tamil తెలుగు - Telugu ไทย - Thai ትግረኛ - Tigrinya Türkçe - Turkish Ukrainian اردو - Urdu ئۇيغۇرچە - Uyghur Ўзбек - Uzbek Việt Nam - Vietnamese Wolof Yao Yorùbá - Yoruba Zarma زولو - Zulu
839 Hadithi
Ensaiklopidia ya Hadithi za Nabii
Makundi
Daraja la hadithi
Imesimuliwa katika
Msimulizi
Kulikuwa na mtu ambaye sifahamu kama kuna mtu alikuwa akiishi mbali kuliko yeye, na swala ilikuwa haimpiti, akaambiwa: Bora ungelinunua Punda ukimpanda nyakati za giza, na unapopita kwenye sehemu ya jangwa. Akasema: "Hainifurahishi nyumba yangu kuwa karibu na Msikiti, mimi ninapenda niandikiwe malipo ya kutembea kwangu, na kurudi kwangu ninaporejea kwa Watu wangu" Akasema Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake: "Hakika Mwenyezi Mungu amekukusanyia malipo yote hayo".
Sahihi Imepokelewa Imamu Muslim
Ya kwamba Haulaa binti Tuwaiti bin Habib bin Asadi bin Abdil-Uzza, alipita kwake akiwa pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake, nikasema: Huyu hapa Haulaa binti Tuwaiti, na wanadai kuwa huwa halali usiku, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake (kwa mshangao): "Halali usiku! hebu chukueni katika matendo kiasi mkiwezacho, na Wallahi ninaapa, Mwenyezi Mungu hachoki mpaka mchoke".
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
"Pindi anapougua mja au akasafiri basi huandikiwa mfano wa yale aliyokuwa akiyafanya akiwa nyumbani tena mwenye afya".
Sahihi Imepokelewa na Al-Bukhaariy
"Kulikuwa na Mfalme mmoja katika wale waliokuwa kabla yenu, na alikuwa na mchawi wake, alipozeeka, akasema kumwambia Mfalme: Hakika mimi nimezeeka, nitumie kijana nitakayemfundisha uchawi, basi akamtumia kijana ili amfundishe, katika njia aliyokuwa akipita kijana huyo kulikuwa na Kasisi basi, siku moja akakaa naye na akasikiliza mazungumzo yake, yakampendeza sana, basi akawa anapokwenda kwa mchawi anapita kwa Kasisi na anakaa kwake, akifika kwa mchawi mchawi anampiga, basi akamlalamikia hilo Kasisi akasema: Ukimuhofia mchawi, basi mwambie nyumbani walinichelewesha, na ukihofia familia yako basi waambie: mchawi alinichelewesha, basi akaendelea katika maisha hayo, mara ghafla alifika mahali akakuta kuna mnyama mkubwa aliyezuia watu kutoka katika shughuli zao, basi akasema: Leo ndio nitajua je, mchawi ndio bora au yule kasisi ndio bora? Akachukua jiwe na akasema: Ewe Mwenyezi Mungu ikiwa suala la huyu Kasisi ndio linapendeka zaidi kwako basi muuwe mnyama huyu, ili watu waendelee na shughuli zao, basi akampiga, akawa kamuua, na watu wakaendelea na shughuli zao, akawa kamuendea Kasisi akamueleza tukio hilo, mchamungu akasema kumwambia: Ee mwanangu basi leo wewe umekuwa bora kuliko mimi, kwa hakika jambo lako limefikia pazuri kwa namna ninavyoona, na kwa hakika utapewa majaribu, ukipewa mateso yoyote basi usimuonyeshe yeyote mahala nilipo, na kijana yule alikuwa akiponya vipofu na wenye ukoma na akiwaponya watu kutokana na maradhi mbali mbali, akazisikia habari hizo mmoja kati ya jamaa wa Mfalme alikuwa amekwishapofuka, basi akamuendea akiwa na zawadi, na akamwambia: Yote unayoyaona hapa ni zawadi yako endapo utaniponyesha. Akasema: Hakika mimi simponyeshi yeyote bali anayeponya ni Mwenyezi Mungu Mtukufu, na endapo utamuamini Mwenyezi Mungu basi nitamuomba Mwenyezi Mungu naye atakuponya, basi yule kipofu akamuamini Mwenyezi Mungu na Mwenyezi Mungu akamponya, basi bwana huyu akaenda kwa Mfalme na akakaa kama alivyokuwa akikaa awali, basi Mfalme kwa mshangao mkubwa akamuuliza: Ni nani aliyekurejeshea macho yako?!! Akasema: Ni Mola wangu Mlezi. Mfalme akasema: Hivi, kwani una mungu mwingine zaidi yangu? Akasema: Mola wangu Mlezi na Mola wako ni Mwenyezi Mungu, akamkamata, na akaendelea kumpa mateso mpaka akamuelekeza mahali alipo yule kijana, basi yule kijana akakamatwa na akaletwa kwa Mfalme, Mfalme akasema kumwambia: Ee mwanangu hivi uchawi wako umefikia kuponya vipofu na wakoma?, na unafanya mambo kadhaa wa kadhaa?. Akasema: Mimi simponyi yeyote, bali anayeponya ni Mwenyezi Mungu, akamkamata akamtesa, akaendelea kumpa mateso mpaka akamuonyesha mahali alipo Kasisi, basi akaletwa yule mchamungu, akaambiwa: Rudi katika dini yako, akakataa, basi Mfalme akaagiza msumeno, akautia msumeno kati kati ya utosi wake, akamchana mpaka upande mmoja wa kiwiliwili chake ukadondoka, kisha akaletwa yule bwana aliyekuwa akikaa pamoja na Mfalme, akaambiwa: Rudi katika dini yako, akakataa, basi akautia msumeno kati kati ya utosi wake, akamchana mpaka upande mmoja wa kiwiliwili chake ukadondoka, kisha akaletwa yule kijana, akaambiwa: Rudi katika dini yako, akakataa, basi akamkabidhi kwa kundi la watu wake, akasema: Mpelekeni katika mlima fulani, kisha pandeni naye mlimani, mkifika keleleni, endapo atarejea katika dini yake basi muacheni, asiporejea basi mrusheni chini, basi wakaenda naye, na wakapanda naye mlimani, akasema: Ewe Mwenyezi Mungu nitosheleze dhidi yao kwa chochote ukitakacho, basi mlima ukawatetemesha na wakaanguka wote, na akarudi kwa Mfalme huku akitembea, Mfalme akasema kumuuliza: Wamefanya nini jamaa zako?! Akasema: Mwenyezi Mungu kanitosheleza dhidi yao. Basi Mfalme akamkabidhi kwa kundi jingine katika watu wake, akasema: Nendeni mkambebe katika mtumbwi, muende naye mpaka mfike naye kati kati ya bahari, basi akikubali kurudi katika dini yake maucheni, asipokubali mtumbukizeni, basi wakaenda naye, akasema: Ewe Mwenyezi Mungu nitosheleze dhidi yao kwa chochote utakacho, basi ule mtumbwi ukawamwaga baharini, na wakaangamia wote, na akarudi kwa Mfalme akiwa anatembea, Mfalme akasema kumuuliza: Wamefanya nini jamaa zako? Akasema: Mwenyezi Mungu kanitosheleza dhidi yao, kisha akasema kumwambia Mfalme: Hakika wewe huwezi kuniua mpaka utekeleze ntakachokuamrisha, akasema: Ni kipi hicho? Akasema: Uwakusanye watu katika uwanja mmoja na unitundike juu ya shina la mti, kisha uchukue mshale mmoja katika ala yangu ya mishale, kisha weka mshale kati kati ya upinde, kisha sema: Bismillaah -Naanza kwa jina la Mwenyezi Mungu- Mola Mlezi wa kijana huyu, kisha nirushie, kwani ukifanya hivyo bila sha utaniua, basi Mfalme akawakusanya watu katika uwanja mmoja, na akamtundika yule kijana juu ya shina la mti, kisha akachukua mshale mmoja kutoka katika ala ya mishale yake, kisha akauweka mshale kati kati ya upinde na akasema: Bismillaah -Naanza kurusha kwa jina la Mwenyezi Mungu- Mola Mlezi wa kijana huyu, kisha akamrushia ukamchoma ule mshale kichwani kwake kati ya jicho na sikio, basi yule kijana akashika kwa mkono wake mahali palipochomwa na mshale akawa amefariki, basi watu wote wakasema kwa sauti moja: Tumemuamini Mola Mlezi wa kijana huyu!. Tumemuamini Mola Mlezi wa kijana huyu!. Tumemuamini Mola Mlezi wa kijana huyu!. Wapambe wakamfuata Mfalme wakamwambia: Unaona ulichokuwa ukikwepa?! Wallahi limetokea ulilokuwa ukilikwepa, tayari watu wote sasa wameamini! Basi Mfalme akaamrisha kuchimbwa Mahandaki, kati kati ya mitaa, basi yakachimbwa, na akakoka moto mkubwa ndani yake, na akasema: Yeyote ambaye hatorejea katika dini yake, basi mchomeni humo, au mwambieni jitose mwenyewe, basi wanajeshi wake wakafanya hivyo, mpaka akaja mwanamke mmoja akiwa na mtoto wake mchanga, basi mama yule akawa mzito sana kujitosa ndani ya moto ule, basi mwanaye yule mchanga akazungumza kumwambia mama yake: Ewe mama yangu kuwa na subira hakika wewe uko katika haki".
Sahihi Imepokelewa Imamu Muslim
"Kila kiungo kwa watu kina sadaka, kila siku inayochomozewa jua: Ukafanya uadilifu kati ya watu wawili ni sadaka, na ukimsaidia mtu katika mnyama wake ukambeba kumpandisha au ukamnyanyulia mzigo wake ni sadaka, na neno zuri ni sadaka, na kwa kila hatua unayokwenda kuelekea msikitini ni sadaka, na ukiondoa maudhi njiani ni sadaka".
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Yalipomfika mauti Abuu Twalib, Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alimjia akamkuta yuko pamoja na Abuu Jahali na Abdallah Bin Umaiyya bin Mughiira, akasema: "Ewe baba yangu mdogo, sema: Laa ilaaha illa llaahu (Hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu) neno ambalo nitakutetea kwalo mbele ya Mwenyezi Mungu", Abuu Jahali akasema: Hivi unataka kuichukia mila ya Abdul Muttwalib (Yaani baba yake) Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akaendelea kumrejelea neno hilo, nao pia wakirudia kumwambia maneno yao, mpaka Abuu Twalib akasema kwa neno lake la mwisho alilowasemesha: Niko katika mila ya Abdul Muttwalib, na akakataa kusema: Laa ilaaha illa llaah, mpokezi anasema: Akasema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Wallahi (Namuapia Allah) nitakuombea msamaha kwa muda wote madam sijakatazwa, Allah akateremsha: "Haifai wala haitakiwi kwa Nabii na wale walioamini kuwaombea msamaha washirikina" [Attauba: 113], Na akateremsha kuhusu Abuu Twalib, akasema kumwambia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Hakika wewe humuongoi umpendaye, lakini Allah anamuongoa amtakaye" [Al-Qasas:56]
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
"Kila kiungo kwa mwanadamu kwake ni sadaka, kila siku linalochomoza jua ndani yake ukafanya uadilifu kati ya watu wawili hiyo ni sadaka, na ukamsaidia mtu katika kipando chake ukambeba au ukamnyanyulia mzigo ni sadaka, na neno zuri ni sadaka, na kila hatua unayopiga kwenda msikitini ni sadaka, na ukiondoa udhia barabarani nisadaka".
Sahihi Imepokelewa na Bukhari na Muslim
Tulikuwa pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika safari, akaondoka kwa ajili ya haja yake, tukaona ndege akiwa na makinda mawili, tukawachukua makinda wake, akaja yule ndege akaanza kupepesa mbawa zake, basi akaja Mtume rehema na amani ziwe juu yake akasema: "Ni nani aliyemuhuzunisha ndege huyu kwa mwanaye? Mrejesheeni mwanaye", na akaona kijiji cha wadudu chungu tulichokichoma kwa moto, akasema: "Hakika hastahiki kuadhibu kwa Moto isipokuwa Mola Mlezi wa Moto".
Sahihi Imepokelewa na Abu Daud