Skip to content
Orodha ya Sura /

التَّكوير

التَّكوير is chapter 81 of the Quran and has 29 verses. This page presents it in full in the Uthmani script, with a verse-by-verse translation of its meaning.

29 Aya Sura Na. 81
Nenda kwenye aya
Kiswahili · Barawani
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

إِذَا ٱلشَّمۡسُ كُوِّرَتۡ

Jua litakapo kunjwa!

Explanation & meanings · 1
  1. Jua litakapo kunjwa na mwangaza wake ukafutwa,

وَإِذَا ٱلنُّجُومُ ٱنكَدَرَتۡ

Na nyota zikazimwa!

Explanation & meanings · 1
  1. Na nyota ikazimwa nuru yao,

وَإِذَا ٱلۡجِبَالُ سُيِّرَتۡ

Na milima ikaondolewa!

Explanation & meanings · 1
  1. Na milima ikaondoshwa hapo ilipo,

وَإِذَا ٱلۡعِشَارُ عُطِّلَتۡ

Na ngamia wenye mimba pevu watakapo achwa wasishughulikiwe,

Explanation & meanings · 1
  1. Na ambao wa kuchukua mimba wakaharibu mimba zao,

وَإِذَا ٱلۡوُحُوشُ حُشِرَتۡ

Na wanyama wa mwituni wakakusanywa!

Explanation & meanings · 1
  1. Na nyama mwitu wakusanywe kutoka vichakani mwao na mashimoni mwao, hawajijui hawajitambui kwa wingi wa kufazaika.