Chuja matokeo
Kadi 335
الموضوعات
الموضوعات (13)
التصنيف الشرعي
Filter ▾
حجم المحتوى3
Jawabu/ Sema: Ni sauti za mashetani wa kijini wanao wapumbaza wajinga ili wajuwe kwamba ni sauti ya maiti alie ombwa ili wawafitinishe na wawapoteze kutokana na dini yao na watu wa makaburini hawasikii wala hawamjibu mwenye kuwaomba au anae waomba kwa ushahidi wa Qur'an Tukufu, anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Kwa hakika wewe huwezi kuwafanya maiti wasikie} (Namli 80) na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Mkiwaomba hawasikii maombi yenu} (Fatwir 14) na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Hukuwa wewe nimwenye kuwafanya wasikie walioko makaburini} (Fatwir 22), sasa hao maiti watawajibu vipi ili hali wao wako katika ulimwengu wa Barzakhi, hawana mafungamano yeyote na watu wa duniani amesema Mwenyezi Mungu {Na nani mpotofu mkubwa kuliko hao wanao waomba, badala ya Mwenyezi Mungu, ambao hawatawaitikia mpaka Siku ya Kiyama na wala hawatambui maombi yao} (Ahqaaf 5).
Jawabu/ sema: wao hawajibu mwenye kuwaita na hawawezi kujibu mwenye kuwaomba au akawaomba nusra, amesema Mwenyezi Mungu: {Na hao mnao waomba badala yake hawamiliki hata ugozi wa kokwa ya tende (13) Mkiwaomba hawasikii maombi yenu; na hata wakisikia hawakujibuni. Na Siku ya Kiyama watakataa ushirikina wenu} (Fatwir 13-14). Hasara ilioje kwa mtu alie danganywa na mashetani na walinganizi wanao potosha waliwapambia ibada za kuwaomba maiti na watu walio zikwa, wakiwemo manabii mawalii na watu wema, amesema Mwenyezi Mungu:{Na nani mpotofu mkubwa kuliko hao wanao waomba, badala ya Mwenyezi Mungu, ambao hawatawaitikia mpaka Siku ya Kiyama na wala hawatambui maombi yao} (Ahqaaf 5).
Jawabu/ Sema: hukumu yake ni shirki kubwa, kwa kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Swali kwa ajili ya mola wako na uchinje} (Kawthar 2) na kauli ya Mwenyezi Mungu: {Sema: Hakika Sala yangu na ibada zangu na uhai wangu na kufa kwangu, ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa viumbe vyote(162) Hana mshirika wake. Na hayo ndiyo niliyo amrishwa na mimi ni wa kwanza wa Waislamu} (Al-Anaam 162-163) na amesema Mtume rehma na amani ziwe juu yake: (Mwenyezi Mungu amemlaani mwenye kukichinjia kisichokuwa Mwenyezi Mungu) Imepokelewa na Imamu Muslim.
Na kuna kanuni inasema: (kile ambacho kinafanyika kwa ajili ya Allah hiyo ni ibada, kukifanyia kisichokuwa Allah ni ushirikina)
Jawabu/ Sema: kufanya hivyo ni shiriki kubwa kwa kauli Mtume rehma na amani ziwe juu yake: (Mwenye kuweka nadhiri ya kumtii Mwenyezi Mungu basi amtii na mwenye kuweka nadhri ya kumuasi Mwenyezi Mungu basi asimuasi) Imepokelewa na imamu Bukhari, nadhiri ni ibada ya kusema na ya kutoa mali au ya kutoa mali au ya kimwili, kulingana na kile alicho kiweka nadhiri na maana ya nadhiri: ni kujilazimisha kufanya jambo ambalo sio lazima kwake kisheria, kwa kutarajia kupata anacho kitarajia au kukinga ambacho ambacho hapendi kimpate, au kwa kushukuru neema iliyo mshukia au janga lililo muondokea nadhiri ni katika ibada ambazo hazijuzu kumfanyia yeyote kinyume cha Mwenyezi Mungu kwasababu Mwenzi mungu amewasifu wenye kutekeleza nadhiri, akasema Mwenyezi Mungu: {Wanatimiza ahadi,na wanaiogopa siku ambayo shari yake inaenea sana} (insan 7)
Na kuna kanuni inasema: kila kitendo ambacho amesifiwa na Mwenyezi Mungu mwenye kukitenda basi kimo katika ibada, kile ambacho ni ibada kumfanyia asiekuwa Mwenyezi Mungu ni Ushirikina.
Jawabu/ Sema: linakuwa wazi jawabu kwa kujua aina tatu za kuomba msaada nazo:
- Kuomba hifadhi kwa kumpwekesha Mwenyezi Mungu kwa kufanya ibada: nako ni kumuomba hifadhi Mwenyezi Mungu kutokana na kila unacho kiogopa. amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Sema: Najikinga kwa Mola Mlezi wa mapambazuko, (1) Na shari ya alivyo viumba, (2)} (Falaqi 1-2) na anasema Mwenyezi Mungu:Sema: Ninajikinga kwa Mola Mlezi wa wanaadamu, (1) Mfalme wa wanaadamu (2) Mungu wa wanaadamu (3) Na shari ya wasiwasi wa Shetani, Khannas}. (Al Nnasi 1-4)
- Ni kuomba hifadhi kwa njia ya halali: nako nikuomba hifadhi kwa viumbe walio hai waliopo na wenye uwezo kukusaidia jambo ulilo waomba na katika yale mambo ambayo yanawezekana kisheria, anasema Mtume rehma na amani ziwe juu yake: Mwenyekupata makimbilio au hifadhi basi na akimbilie huko) Imepokelewa na Imamu Muslim.
3-Kuomba hifadhi kwa njia ya ushirikina: nako ni kukiomba hifadhi kisichokuwa Mwenyezi Mungu katika mambo ambayo hakuna anae yaweza ila ni Mwenyezi Mungu, amesema Mwenyezi Mungu: {Na hakika walikuwako wanaume katika watu walio kuwa wakitafuta kujikinga kwa wanaume wa kijini; kwa hivyo wakawazidisha madhambi} Jinni 6
Jawabu/ Sema: Ninasema yale aliyo niongoza Mtume wa Allah rehma na amani za Allah ziwe juu yake, alisema: (Mwenye kufika katika nyumba yeyote akasema: Ninajikinga kwa maneno ya Mwenyezi Mungu yalio timia kutokana na shari alizo ziumba, hakuna kitakacho mdhuru mpaka atakapo toka katika nyumba hiyo) Imepokelewa na Muslim
Jawabu/ Sema: kufanya hivyo nikatika ushirikina mkubwa unao tengua matendo ya mwanadamu na unao mtuoa mtu katika dini na kumfanya aishi milele katika moto kwa yule atakae ufanya na hakutubia kabla ya kufa, kwa kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Nani yule anaye mjibu mwenye shida pale anapo mwomba na akaiondoa dhiki} (Namli 62) Maana yake ni kwamba hakuna mwenye uwezo wa kumjibu ila ni Mwenyezi Mungu na hakuna mwenye kuondosha madhara ila ni Mwenyezi Mungu. akawakamea Mwenyezi Mungu kila mwenye kuomba nusra kwa asie kuwa yeye kwa kuanza maneno yake kwa kuuliza, kwa sababu kuomba nusra ni kufanya ibada vilevile kuomba msaada, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Kumbukeni wakati mkiomba nusra kwa Mola wenu mlezi} (Anfal 9) na imethibiti katika sahihi bukhari kutoka kwa Abuu Hurayrah radhi za Allah ziwe juu yake kwamba hakika Mtume rehma za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake alisema: nisimkute mmoja wenu atakae kuja siku ya Kiyama akiwa na ngamia anaetoa sauti ya juu, kisha akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu niokoe na ninusuru, ispokuwa nitasema: tayari nimesha kufikishia hakika mimi similiki chochote katika hilo unalo niomba, nisimkute mmoja wenu anakuja siku ya qiyama akiwa na farasi anaetoa sauti ya chini, kisha anasema: ewe mtume niokowe, nitasema similiki chochote kwa Mwenyezi Mungu nimesha kufikishia, Imepokelewa na Bukhari na Muslim. na ijulikane wazi kuwa inajuzu kuomba nusra kwa wanadamu walio hai ambao tunawaona, sio wale ambao hawapo ikiwa ni katika mambo anayo na uwezo nayo na kuomba nusra kwa mwanadamu allie hai ina maana ya kumuomba msaada, katika yale anayo yaweza kiumbe, kama alivyo omba rafiki wa mussa kwa mussa amsaidie kutokana na adui yao, amesema Allah Mtukufu: {Yule mwenzake alimtaka msaada kumpiga adui yake} (Qaswaswi15) ama kuomba nusra kwa wasiokuwepo miongoni mwa watu na majini na watu wa makaburini wanachuoni wamekubaliana kuwa niharam na nibatili na nikatika Ushirikina.
Jawabu/ sema: Haijuzu kwani wanachuoni wamekubaliana juu ya uharamu wa kila jina linalo abudiwa kinyume cha Mwenyezi Mungu na ni wajibu kubadilisha jina linalo abudiwa kinyume cha Mwenyezi Mungu, kama jina: Mja wa Nabii, mja wa Mtume, mja wa Hussein na mja wa Al Kaaba na majina mengine mfano wa majina hayo na majina bora na yanayo pendeza kwa Mwenyezi Mungu ni: (Abdullah na Abdurahmani) kama ilivyo kuja katika hadithi sahihi kutoka kwa Mtume rehma na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: (Hakika majina yanayo pendeza zaidi kwa Mwenyezi Mungu ni Abdullah na Abdurahmani) Imepokelewa na Imamu Muslim. ni wajubu kubadilisha majina yanayo abudiwa kinyume na Mwenyezi Mungu na hii ni kwa wale waliopewa majina hayo na wapo hai walio itwa majina yanayo abudiwa kinyume cha Mwenyezi Mungu.
Jawabu/ sema: kufanya hivyo ni ushirikina kwa dalili ya maneno ya Mtume -rehma na amani ziwe juu yake-: (mwenye kuvaa hirizi atakuwa amemshirikisha Mwenyezi Mungu) Imepokelewa na Imamu Ahmad katika kitabu chake na amesema Mtume -rehma na amani ziwe juu yake-( Isibakishwe katika shingo la ngamia kamba itokanayo na mshale au hirizi lolote ila imekatwa) Imepokelewa na imamu bukhari. na kauli ya Mtume -rehma na amani ziwe juu yake-: (Mwenye kusuka ndevu zake au akavaa kamba ya upinde shingoni au akastanji kwa choo cha mnyama au mfupa hakika Muhammad yuko mbali nae) Imepokelewa na Abuu Daudi, na amesema Mtume -rehma na amani ziwe juu yake-:(Mwenye kuvaa hirizi Mwenyezi Mungu asimtimizie mambo yake) Imepokelewa na Ibn Hibaani katika sahihi yake. Ameenda patupu mwenye kutegemea vitu vya upuuzi na uzushi, imekuja katika hadithi: (Mwenye kukitegemea kitu au kukivaa basi ataaegemezewa kwa kitu hicho kimsaidie).
Tiwala: Ni uchawi unaofanywa wakiitakidi kuwa inamfanya mume ampende mke wake, au unawatenganisha na wanafanya uchawi huo kwa lengo la kuleta chuki baina ya wapendanao na watu wakaribu.
Hirizi: ni kitu kinacho vishwa watoto kwa kuzuia kijicho na hasadi
Na maana ya Mahirizi, amesema Almundhiry: (Mahirizi walikuwa wanayavaa wakiona kuwa yanaepusha maafa mbali mbali) na huu ni ujinga na ni upotevu, kwa sababu sio sababu wala sio sheria kufanya hivyo wala sio Qadar na kuvaa hirizi kunakusanya kuvaa bangili na kuninginiza vitambaa kwa lengo la kuzuia mabalaa na kuleta manufaa kwa mtu, myama gari na nyumba.
Jawabu/ Sema: Kutaka baraka kumegawanyika mara mbili:
- Kutaka baraka ambako kuna swihi kisheria ambako kumeruhusiwa na Qur'an na Sunnahh juu ya kuswihi kwake na kunufaika mwenye kufanya hivyo na haiswihi kuitakidi kuwepo baraka katika jambo ila iwe ni kwa dalili zilizo thibiti katika Qur'an na Sunnahh, akili haina nafasi katika hilo wala kuliona jambo kuwa linapendeza kufanya hivyo, hatujui kuwa jambo hili kuna baraka ndani yake ila kwa maelezo kutoka kwa muumbaji mwenye hekima mwenye baraka na alie tukuka, au kwa maelezo kutoka kwa Mtume -rehma na amani ziwe juu yake- kutokana na vitu ambavyo vimetokana na yeye kama vile, nywele na mavazi yake na haya ni maalumu kwa Mtume -rehma na amani ziwe juu yake- na yale yalio thibiti kuwa ameambatana nayo kama nywele na mavazi na watu wazushi wanasema uongo na wanadai kuwa wana nywele za Mtume na nguo zake na haya yote wanayafanya kwa ajili ya kuzichezea akili za baadhi ya waislam na kuharibu dini yao nakuchukuwa dunia yao.
- Sehemu ya pili: kutaka baraka kuliko katazwa na ilio haramu, ni ile inayo mfikisha mtu katika kumshirikisha Mwenyezi Mungu kama vile kutaka baraka kwa watu wema na vile vinavyo tokana nawao na kutaka baraka kwa makaburi yao kwa kuswali katika makaburi au kuwaomba wakiwa makaburini na kutaka baraka kwa michanga yao kwa kuitakidi kuwa mchanga huo ni dawa na mfano wake ni kutaka baraka na kufanya twawafu au kuvaa vitambaa kwa kila sehemu na mawe na miti akiitakidi kuwa vina ubora na imejulikana kuwa haipatikani chochote kinacho eleza kuwa nisheria kukibusu na kukigusa ila ni jiwe leusi lililopo katika alkaaba na nguzo zake na visivyokua hivyo nimakosa kufanya hivyo kuvigusa na kubusu na kufanya twawafu na kufanya hivyo ni shirki kubwa kwa mwenye kuitakidi kuwa vinaleta baraka vyenyewe, au ni katika shirki ndogo kwa mwenye kudai kuwa ni sababu ya baraka.
Jwabu/ sema: Hii ni itikadi na ibada iliyo zushiwa kwa sababu Maswahaba wa Mtume wetu Muhammad -rehma na amani ziwe juu yake- walikuwa ni wajuzi zaidi na niwatu bora, na niwenye ufahamu zaidi na wanabidii kubwa katika kufanya kheri na niwajuzi wa mambo bora kwa watu wa ubora, hawakutabaruku kwa athari za Abubakari, Omar, Othman na Ally -radhi za Allah ziwe juu yao- na hawakufatilia athari zao ili kutafuta baraka kwao ilihali wao ni watu bora katika Umma huu baada ya manabii, kwa sababu wao walijua kuwa kufanya hivyo ni makosa, na Omar -radhi za Allah ziwe juu yake- alikata mti uliofanyiwa mapatano yalio ridhiwa (Baiatu ridhwan) kwa kuchelea watu wasichupe mipaka kwenye mti huo, na watu wema walio tangulia wao ndio wenye pupa zaidi ya kufanya kheri na laiti ingekuwa kufuata athari za watu wema walio tangulia ni bora basi wangetutangulia kufanya hivyo.
Jawabu/ Jawabu: Kufanya hivyo nikatika Ushirikina, imepokelewa kutoka kwa Imamu Ahmad na Tirmidhiy kutoka kwa Abi Waaqid Allaythiy alisema: Tulitoka pamoja na Mtume rehma na amani ziwe juu yake kwenda khunayni na sisi tukiwa ni waislam wapya na washirikina walikuwa na Mti wa Mkunazi wakiketi chini yake kwa ajili ya kuomba na kutundika silaha zao, Mti huo unaitwa dhatu anwat (Mti wanao tundika juu yake Silaha zao) mara tukapita kwenye Mti wa Mkunazi mwingine tukamwambia Mtume -rehma na amani ziwe juu yake- akawajibu Mtume -rehma na amani ziwe juu yake-: (Allah ni Mkubwa hakika hilo mlilo sema ni mwenendo wa watu wajinga walio pita, nina muapa Allah ambae nafsi yangu iko mikononi mwake, hayo mliyosema ni sawa na yale waliyo sema wana wa Izrael kumwambia Mussa: {Tuwekee waungu tuwaabudu kama makafiri walivyo na miungu, Musa akasema hakika nyinyi ni watu wajinga} (A'araf 138) mtazidi kufuata myenendo ya watu waliokuwa kabla yenu).
Jawabu/ Sema: Haijuzu kukiapia kisichokua Mwenyezi Mungu Mtukufu, Amesema Mtume rehma na amani ziwe juu yake: (Atakae kuwa ni mwenye kuapa basi aapie kwa jina la Mwenyezi Mungu) Imepokelewa na Bukhari. Mtume rehma na amani ziwe juu yake alikataza kuapia kisichokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, kama ilivyo kuja katika kauli ya mtume rehma na amani ziwe juu yake: (Msiapie kwa majina ya wazazi wenu wala kwa majina ya Matwaghuti) Imepokelewa na Muslim na Matwaghuti: -ni kila kinacho abudiwa kinyume cha Allah, kikiwa kimeridhia au kiongozi asie fuata sheria za Allah au sheria zozote zisizokuwa za Allah- bali mtume rehma na amni ziwe juu yake alijalia kufanya hivyo ni katika shirki, kama ilivyo katika kauli yake Mtume rehma na amani ziwe juu yake: (Mwenye kukiapia kisichokuwa Mwenyezi Mungu atakuwa amekufuru au amemshirikisha Mwenyezi Mungu) na amesema Mwenyezi Mungu: (Mwenyekuapia kwa uaminifu wake atakuwa sio katika sisi) Imepokelewa na Imamu Ahmad na Ibn Hibani ma Hakim kwa upokezi sahihi.
Muislam ajitahadhari na kuapia kwa jina la Mtume au walii, au kuapia kwa cheo amana na Alkaaba,na mengineyo katika viumbe vya Mwenyezi Mungu.
Jawabu/ sema: Haijuzu kuitakidi hivyo kwasababu hivyo havina athari yeyote hata na hakuna wanao sadikisha hayo ila ni watu wenye akili dhaifu, wanaofuata mambo ya kipuuzi na kuitakidi hivyo ni katika ushirikina kwa kauli ya mtume rehma na amni ziwe juu yake katika hadithi Alqudsiyu: (Hakika Mwenyezi Mungu anasema: mwenye kusema mvua imenyesha kwa fadhila za Mwenyezi Mungu na rehma zake, basi mtu huyo ni mwenye kuniamini na ni mwenye kukufuru uwezo wa nyota na sayari na mwenye kusema Mvua imenyesha kwa sababu ya watu fulani na kwasababu fulani basi huyo atakuwa amenikufuru na anaamini kuwa nyota na sayari zingine zina uwezo wa kudhuru na kunufaisha) Imepokelewa na Bukhari na Muslim na watu wa enzi za ujinga walikuwa wanaitakidi kuwa nyota zina athari katika kunyesha Mvua.