Skip to content

utakapo ulizwa: Je inajuzu kuitakidi kuwa nyota au sayari zingine zina athari juu ya ulimwengu na watu katika kuleta manufaa na tawfiiki na mafanikio, au kuzuia shari na mambo yanayo chukizwa na Mabalaa.

السؤال

Swali/ utakapo ulizwa: Je inajuzu kuitakidi kuwa nyota au sayari zingine zina athari juu ya ulimwengu na watu katika kuleta manufaa na tawfiiki na mafanikio, au kuzuia shari na mambo yanayo chukizwa na Mabalaa.

الجواب

Jawabu/ sema: Haijuzu kuitakidi hivyo kwasababu hivyo havina athari yeyote hata na hakuna wanao sadikisha hayo ila ni watu wenye akili dhaifu, wanaofuata mambo ya kipuuzi na kuitakidi hivyo ni katika ushirikina kwa kauli ya mtume rehma na amni ziwe juu yake katika hadithi Alqudsiyu: (Hakika Mwenyezi Mungu anasema: mwenye kusema mvua imenyesha kwa fadhila za Mwenyezi Mungu na rehma zake, basi mtu huyo ni mwenye kuniamini na ni mwenye kukufuru uwezo wa nyota na sayari na mwenye kusema Mvua imenyesha kwa sababu ya watu fulani na kwasababu fulani basi huyo atakuwa amenikufuru na anaamini kuwa nyota na sayari zingine zina uwezo wa kudhuru na kunufaisha) Imepokelewa na Bukhari na Muslim na watu wa enzi za ujinga walikuwa wanaitakidi kuwa nyota zina athari katika kunyesha Mvua.