Utakapo ulizwa: Je, Kufuata athari za watu wema na kutabaruku kwa dhati zao na athari zao ni jambo ambalo lipo kisheria au ni uzushi na upotovu?
السؤال
Swali/ Utakapo ulizwa: Je, Kufuata athari za watu wema na kutabaruku kwa dhati zao na athari zao ni jambo ambalo lipo kisheria au ni uzushi na upotovu?
الجواب
Jwabu/ sema: Hii ni itikadi na ibada iliyo zushiwa kwa sababu Maswahaba wa Mtume wetu Muhammad -rehma na amani ziwe juu yake- walikuwa ni wajuzi zaidi na niwatu bora, na niwenye ufahamu zaidi na wanabidii kubwa katika kufanya kheri na niwajuzi wa mambo bora kwa watu wa ubora, hawakutabaruku kwa athari za Abubakari, Omar, Othman na Ally -radhi za Allah ziwe juu yao- na hawakufatilia athari zao ili kutafuta baraka kwao ilihali wao ni watu bora katika Umma huu baada ya manabii, kwa sababu wao walijua kuwa kufanya hivyo ni makosa, na Omar -radhi za Allah ziwe juu yake- alikata mti uliofanyiwa mapatano yalio ridhiwa (Baiatu ridhwan) kwa kuchelea watu wasichupe mipaka kwenye mti huo, na watu wema walio tangulia wao ndio wenye pupa zaidi ya kufanya kheri na laiti ingekuwa kufuata athari za watu wema walio tangulia ni bora basi wangetutangulia kufanya hivyo.