Skip to content

Utakapo ulizwa: nikipi ambacho kinacho sikika makaburini kwa baadhi ya walio kufa ambao wanatukuzwa na baadhi ya wajinga?

السؤال

Swali/ Utakapo ulizwa: nikipi ambacho kinacho sikika makaburini kwa baadhi ya walio kufa ambao wanatukuzwa na baadhi ya wajinga?

الجواب

Jawabu/ Sema: Ni sauti za mashetani wa kijini wanao wapumbaza wajinga ili wajuwe kwamba ni sauti ya maiti alie ombwa ili wawafitinishe na wawapoteze kutokana na dini yao na watu wa makaburini hawasikii wala hawamjibu mwenye kuwaomba au anae waomba kwa ushahidi wa Qur'an Tukufu, anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Kwa hakika wewe huwezi kuwafanya maiti wasikie} (Namli 80) na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Mkiwaomba hawasikii maombi yenu} (Fatwir 14) na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Hukuwa wewe nimwenye kuwafanya wasikie walioko makaburini} (Fatwir 22), sasa hao maiti watawajibu vipi ili hali wao wako katika ulimwengu wa Barzakhi, hawana mafungamano yeyote na watu wa duniani amesema Mwenyezi Mungu {Na nani mpotofu mkubwa kuliko hao wanao waomba, badala ya Mwenyezi Mungu, ambao hawatawaitikia mpaka Siku ya Kiyama na wala hawatambui maombi yao} (Ahqaaf 5).