Utakapo ulizwa: ipi hukumu ya kukichinjia kisichokuwa Mwenyezi Mungu kwa lengo la kujikurubisha kwa kilicho chinjiwa?
السؤال
Swali/ Utakapo ulizwa: ipi hukumu ya kukichinjia kisichokuwa Mwenyezi Mungu kwa lengo la kujikurubisha kwa kilicho chinjiwa?
الجواب
Jawabu/ Sema: hukumu yake ni shirki kubwa, kwa kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Swali kwa ajili ya mola wako na uchinje} (Kawthar 2) na kauli ya Mwenyezi Mungu: {Sema: Hakika Sala yangu na ibada zangu na uhai wangu na kufa kwangu, ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa viumbe vyote(162) Hana mshirika wake. Na hayo ndiyo niliyo amrishwa na mimi ni wa kwanza wa Waislamu} (Al-Anaam 162-163) na amesema Mtume rehma na amani ziwe juu yake: (Mwenyezi Mungu amemlaani mwenye kukichinjia kisichokuwa Mwenyezi Mungu) Imepokelewa na Imamu Muslim.
Na kuna kanuni inasema: (kile ambacho kinafanyika kwa ajili ya Allah hiyo ni ibada, kukifanyia kisichokuwa Allah ni ushirikina)