Utakapo ulizwa: Ni ipi hukumu ya kuvaa bangili, au uzi mkononi au shingoni au kumvisha Mnyama au gari au sehemu nyingine kwa ajili ya kuzuia kijicho au husda, au kuondoa mabalaa na shari?
السؤال
Swali/ Utakapo ulizwa: Ni ipi hukumu ya kuvaa bangili, au uzi mkononi au shingoni au kumvisha Mnyama au gari au sehemu nyingine kwa ajili ya kuzuia kijicho au husda, au kuondoa mabalaa na shari?
الجواب
Jawabu/ sema: kufanya hivyo ni ushirikina kwa dalili ya maneno ya Mtume -rehma na amani ziwe juu yake-: (mwenye kuvaa hirizi atakuwa amemshirikisha Mwenyezi Mungu) Imepokelewa na Imamu Ahmad katika kitabu chake na amesema Mtume -rehma na amani ziwe juu yake-( Isibakishwe katika shingo la ngamia kamba itokanayo na mshale au hirizi lolote ila imekatwa) Imepokelewa na imamu bukhari. na kauli ya Mtume -rehma na amani ziwe juu yake-: (Mwenye kusuka ndevu zake au akavaa kamba ya upinde shingoni au akastanji kwa choo cha mnyama au mfupa hakika Muhammad yuko mbali nae) Imepokelewa na Abuu Daudi, na amesema Mtume -rehma na amani ziwe juu yake-:(Mwenye kuvaa hirizi Mwenyezi Mungu asimtimizie mambo yake) Imepokelewa na Ibn Hibaani katika sahihi yake. Ameenda patupu mwenye kutegemea vitu vya upuuzi na uzushi, imekuja katika hadithi: (Mwenye kukitegemea kitu au kukivaa basi ataaegemezewa kwa kitu hicho kimsaidie).
Tiwala: Ni uchawi unaofanywa wakiitakidi kuwa inamfanya mume ampende mke wake, au unawatenganisha na wanafanya uchawi huo kwa lengo la kuleta chuki baina ya wapendanao na watu wakaribu.
Hirizi: ni kitu kinacho vishwa watoto kwa kuzuia kijicho na hasadi
Na maana ya Mahirizi, amesema Almundhiry: (Mahirizi walikuwa wanayavaa wakiona kuwa yanaepusha maafa mbali mbali) na huu ni ujinga na ni upotevu, kwa sababu sio sababu wala sio sheria kufanya hivyo wala sio Qadar na kuvaa hirizi kunakusanya kuvaa bangili na kuninginiza vitambaa kwa lengo la kuzuia mabalaa na kuleta manufaa kwa mtu, myama gari na nyumba.