Chuja matokeo
Kadi 335
الموضوعات
الموضوعات (13)
التصنيف الشرعي
Filter ▾
حجم المحتوى3
Jawabu/ Sema: Ni Ushirikina amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:{Hakika wamekufuru walio sema: Mwenyezi Mungu ni Masihi mwana wa Maryamu! Na hali Masihi mwenyewe alisema: Enyi Wana wa Israili! Muabuduni Mwenyezi Mungu, Mola wangu Mlezi na Mola wenu Mlezi. Kwani anaye mshirikisha Mwenyezi Mungu, hakika Mwenyezi Mungu atamharamishia Pepo na mahala pake ni Motoni. Na walio dhulumu hawatakuwa na wa kuwanusuru} (Al-Maida 72) na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Hakika Mwenyezi Mungu hasamehi kushirikishwa na husamehe yaliyo duni ya hilo kwa amtakaye} (Annisaa 48) kitendo cha kuwa Mwenyezi Mungu hasamehi dhambi za Mshirikina akifa hajatubia ni alama kuwa Shirki ni dhambi kubwa, kinacho bainisha hilo ni kauli ya Mtume rehma na amani ziwe juu yake pindi alipo ulizwa: ni ipi dhambi kubwa? akasema Mtume rehma na amani ziwe juu yake: (ni kumfanya Mwenyezi Mungu kuwa ana msaidizi wake au mfano wake katika viumbe ilihali yeye amekuumba...) Imepokelewa na Bukhari na Muslim.
Ushirikina: Ni Mtu kumjalia Mwenyezi Mungu kuwa na msaidizi wake ambae wako sawa katika kazi zake au anayo sifa miongoni mwa sifa zake, katika Malaika au Mtume au Walii namfano wake, anaamini kuwepo chochote kwa kiumbe huyo katika sifa za Mwenyezi Mungu na mambo yanayo Muhusu yeye ikiwemo kuumba au ufalme au kupangikia mambo yoote ya wajawake, au akajikurubisha kwake akawa anamuomba, au kumtarajia, au kumuogopa, au anategemea, au anataka kwake kinyume cha Mwenyezi Mungu au pamoja na Mwenyezi Mungu, akakifanyia chochote katika aina za ibada za mali au mwili za dhahiri au zilizo jificha.
Jawabu/ Sema: Ushirikina umegawanyika mara mbili:
1.Shirki Kubwa: Nayo ni kukifanyia ibada kisichokuwa Mwenyezi Mungu, Kama kutegemea kwa asiekuwa Mwenyezi Mungu, au kuomba msaada kwa walio kufa, au kukichinjia kisichokuwa Mwenyezi Mungu, au kutoa nadhiri kwa kisichokuwa Mwenyezi Mungu, au kukisujudia kisichokuwa Mwenyezi Mungu, au kuomba nusra kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu katika mambo ambayo hakuna mwenye uwezo nayo ila ni Mwenyezi Mungu, kama kuomba nusra kwa wasio kuwepo, au walio kufa na hakuna anaefanya mambo haya ya kijinga ila mwenye kuitakidi uwezo wao wa kujibu na kwamba wana uwezo wa kufanya mambo ambayo hakuna mja anaweza kufanya ila ni Mwwnyezi Mungu, anakuwa kwa kitendo hicho ameitakidi kwa kiumbe huyo kuwa na mambo yanayo muhusu Mwenyezi Mungu, anakinyenyekea na kujidhalilisha kwake udhalili wa kukiabudu na anakitegemea katika mambo yake na anaomba nusra kwa kitu hicho na anakiita akiomba mambo ambayo hakuna kiumbe anaeweza kumtimizia. Na jambo la ajabu ni mtu kuomba nusra kwa kitu ambacho hakina uwezo wowote hakimiliki kujiletea manufaa wala kujikinga na Madhara, hakimiliki kifo wala uhai wala kufufuliwa na mtu ambae hawezi kujiletea manufaa wala kuzuia madhara juu ya nafsi yake vipi atamiliki vitu hivyo kwa watu wengine, kitendo hiki ni kama mfano wa mtu anae zama baharini kumuomba msaada mwenzake ambae anazama.Utakasifu ni wa Mwenyezi Mungu! Vipi yamefunga macho ya washirikina na kuondoka kwa akili zao wakadiriki kufanya Ushirikina unaopingana na sheria ya Mwenyezi Mungu, Ushirikina unao pingana na akili salama, pia Ushirikina unao pingana na Maumbile!
2.Shirki ndogo: Mfano wa kujionyesha kama alivyo sema Mtume rehma na amani ziwe juu yake: (Jambo kubwa ambalo ninalo chelea kwenu ni Shirki ndogo, akaulizwa kuhusu shirki ndogo akasema: Kujionyesha (Riyaa) Imepokelewa na Muslim na mfano mwingine wa shirki ndogo ni kuapia kwa kisichokuwa Mwenyezi Mungu, amesema Mtume rehma na amani ziwe juu yake: (Mwenyekuapia kisichokuwa Mwenyezi Mungu atakuwa amekufuru au amefanya shirki) Imepokelewa na Tirmidhy.
Jawabu/ Sema: Ukafiri upo aina mbili:
1.Ukafiri mkubwa: unamtoa mtu katika uislam nao ni wenye kupingana na uislam kama mwenye kumtukana Allah au mtume wake au dini yake au akafanya masihara au istihzai katika sheria ya uislam au akaikataa habari ya Allah au amri yake au makatazo yake, akakadhibisha yale aliyoyaeleza Allah na mtume wake au akakanusha chochote alicho kifaradhisha Allah kwa waja wake, Au akahalalisha aliyoharamisha Allah na mtume wake. Amesema Allah mtukufu: (Sema: Mlikuwa mkimfanyia masihara Mwenyezi Mungu na ishara zake na Mtume wake? (65) Msitoe udhuru; mmekwisha kufuru baada ya kuamini kwenu! Tukilisamehe kundi moja kati yenu, tutaliadhibu kundi jingine kwa kuwa wao ni wakosefu) (Tauba 65-66.)
2.Ukafiri mdogo nao ni ule ambao dalili za kisheria zimeuita ni ukafiri na sio ukafiri mkubwa kwa jina jingine unaitwa kukufuru neema au ukafiri mdogo, kama vile muislamu kupigana na muislamu mwenzake, kujivua unasabu na kuomboleza na mfano wake katika mambo ya kijinga amesema mtume rehma na amani ziwe juu yake (kumtukana muislamu ni uovu na kupigana naye ni ukafiri) Imepokelewa na Bukhar, amesema mtume rehma na amani ziwe juu yake: (watu wa aina mbili katika watu wana ukafiri: mwenye kutia dosari kwa nasabu na kuomboleza kwa maiti), imepokelewa na Muslim: Ibada hizi hazimtoi mtu katika Uislam lakini ni katika madhambi makubwa Allah atuepushe.
Jawabu/ sema: Unafiki upo aina mbili, Unafiki mkubwa na unafiki mdogo.
Unafiki mkubwa: ni kudhihirisha Uislam na kuficha ukafiri na hizi ni katika hathari zake kubwa kuuchukia uislam na kuuchukia ushindi wake na kuwachukia waislam na kufanya bidii ya kuwapiga vita na kuharibu dini yao.
Unafiki mdogo ni kujifananisha na vitendo vya wanafiki bila kuficha ukafiri, kama mfano anayesema uwongo anapoongea na anapo ahidi hatimizi na anapo aminiwa anafanya hiyana, amesema Mtume rehma na amani ziwe juu yake (Alama za mnafiki ni tatu, Akiongea anasema uongo, akiaminiwa anafanya hiyana na anapo ahidi hatimizi)Imepokelewa na Imamu Bukhar.
Jawabu/ sema: Chenye kutengua maana yake ni chenye kubatilisha na chenye kuharibu, Wakati wowote kinapotokea kwenye jambo uharibu, kama vile vibatilisho vya udhu ambavyo mwenye kuvifanya vinambatilisha udhu na analazimika kutawadha tena, mfano wake ni mfano vinavyobatilisha uislamu, mja anapovifanya uislam wake unaharibika na kubatilika na mtendaji anatoka katika uislamu na kuwa kafiri na wana wa chuoni wametaja katika mlango wa kuritadi na hukmu za mwenye kuritadi wametaja aina nyingi za vitu ambavyo vinaweza kumfanya Muislamu akaritadi na kutoka katika dini yake ikawa halali damu yake na mali yake na vitu vyenye hatari zaidi na vikubwa na nivingi kwa kutokea na vile ambavyo wanakubaliana wana wa chuoni kuwa vinatengua, ni vitenguzi kumi navyo: 1:Kumshirikisha Allah katika Ibada amesema Allah mtukufu: (Hakika Mwenyezi Mungu hasamehi kushirikishwa na kitu. Lakini Yeye husamehe yasiyo kuwa hayo kwa amtakaye. Na anaye mshirikisha Mwenyezi Mungu basi huyo amepotea upotovu wa mbali.) (Annisai 116). Na amesema Allah mtukufu {Kwani anaye mshirikisha Mwenyezi Mungu, hakika Mwenyezi Mungu atamharimishia Pepo na mahala pake ni Motoni. Walio dhulumu hawatakuwa na wa kuwanusuru.} (Almaida 72), miongoni mwa kumshirikisha mwenyezi Mungu katika Ibada ni kuviomba visivyo kuwa Allah na kuviomba nusra na kujikinga kwavyo na kuweka nadhiri na kuvichinjia, kama anayemchinja jini au kaburi au walii akiwa hai au hakuwa maiti kwa lengo la kuleta manufaa au kuzuia shari kama wanavyofanya wajinga wanaidanganywa kwa uongo na shubha za waganga waongo na watu wa mazingara.
2: Mwenye kujalia baina yake na baina ua Allah wasaidizi akiwaomba kupona na kumtegemea katika kupata matakwa yake na wanawategemea katika kupata mahitaji yake ya kidunia na ya akhera, mtu huyo itakuwa amekufuru kwa makubaliano ya wana wa chuoni ,amesema Allah mtukufu): (sema hakika mimi ninamuomba mola wangu na simshirikishi na chochote) (Al Jinni 20).
3. Mtu ambae hakukufurisha washirikina au akatilia shaka katika ukafiri wao, au akasahihisha madhehebu yao ya ukafiri. Amesema Allah Mtukufu: {Na Mayahudi wanasema: Uzeir ni mwana wa Mungu. Na Wakristo wanasema: Masihi ni mwana wa Mungu. Hiyo ndiyo kauli yao kwa vinywa vyao. Wanayaiga maneno ya walio kufuru kabla yao. Mwenyezi Mungu awaangamize! Wanageuzwa namna gani hawa!} (Tawba 30) kwasababu kuridhia ukafiri ni ukafiri na dini haiswihi dini ispokuwa kwa kukufuru vyote vinavyo abudiwa kinyume cha Allah.(Twaghuti) na kuitakidi ubatili wa dini zote zisizokuwa uislam na kuzichukia na kujitakasa kutokana na dini hizo na wafuasi wa hizo dini na kupigana nao kwa kadri ya uwezavyo.
- Mwenye kuitakidi kwamba uongofu usiokuwa wa Mtume rehma na amani ziwe juu yake, ndio ulio kamilika kuliko uongofu wake, au akaitakidi kwamba hukumu ya asiyekuwa mtume ndio nzuri kuliko hukumu yake, Kama mfano wa yule anae fadhilisha hukumu za Matwaghuti na sheria za viumbe kuwa ndio bora kuliko sheria za Allah na Mtume wake, amesema Allah Mtukufu: {La! Naapa kwa Mola wako Mlezi! hawataamini mpaka wakufanye wewe ndiye muamuzi katika yale wanayo hitalafiana, kisha wasione uzito katika nyoyo zao juu ya hukumu utayo toa na wanyenyekee kabisa} (Nisaai 65). Mwenye kutanguliza kauli za Mashekh wa upotevu na mambo yao ya kizushi juu ya sunnahh za Mtume zilizo sahihi akiwa anajua akiwa anajua kuwa hizo sunnahh zimethibiti kuwa ni zamtume, Mwenyekufanya hivyo atakuwa ni kafiri kwa ijimai ya wanachuoni.
5.Mwenye kuchukia chochote katika mambo aliyo kuja nayo Mtume rehma na amani ziwe juu yake, Hatakama atayafanyia kazi, akiyachukia atakuwa amekufuru, Amesema Allah mtukufu: {Hayo ni kwa sababu waliyachukia aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu, basi akaviangusha vitendo vyao}. (Muhammad 9).
- Mwenye kufanya masihara na dini aliyo kuja nayo Mtume rehma na amani ziwe juu yake, kama mwenye kufanya mzaha na baadhi ya sheria zake na hukumu zake na sunnahh zake na yale aliyo yaeleza, au anafanya masihara na yale aliyo yaeleza Mtume katika malipo ya waja watakao fanya mema, au adhabu kwa wenye kufanya Maasi katika yale aliyo yaeleza Mtume rehma na amani ziwe juu yake, mwenye kufanya masihara na hayo yalio tajwa atakuwa amekufuru na ushahidi ni Kauli ya Allah Mtukufu: {(Sema: Mlikuwa mkimfanyia masihara Mwenyezi Mungu na ishara zake na Mtume wake? Msitoe udhuru; mmekwisha kufuru baada ya kuamini kwenu! Tukilisamehe kundi moja kati yenu, tutaliadhibu kundi jingine kwa kuwa wao ni wakosefu) } (Tawba 65-66)
- Uchawi na hauwi ila kwa kutumia majini na mashetani na kuwashirikisha na kufanya mambo ambayo ni yaukafiri, kwa sababu ya kupata radhi zao, miongoni mwa uchawi nikufanya jambo la ajabu lenye kuathiri hisia za watu mwenye kufanya mamno hayo au akaridhia atakuwa amekufuru na ushahidi ni kauli ya Allah Mtukufu: {Wala hao hawakumfundisha yeyote mpaka wamwambie: Hakika sisi ni mtihani; basi usikufuru}. ( Al Baqara 102).
8.Ni kujumuika na washirikina na kuwasaidia ili wawashinde waislam na dalili ni kauli ya Allah Mtukufu {Na miongoni mwenu mwenye kufanya urafiki nao, basi huyo ni katika wao. Hakika Mwenyezi Mungu hawaongoi watu wenye kudhulumu} (Al Maidah 51).
9.Mwenye kuitakidi kwamba baadhi ya waislam wanaruhusiwa kutoka katika sheria ya Muhammad rehma na amani ziwe juu yake kama Hidhri alivyo toka katika baadhi ya sheria ya nabii Musa rehma ziwe juu yake, mwenye kuitakidi hivyo atakuwa kafiri. dalili ni kauli ya Allah Mtukufu : {Na anaye tafuta dini isiyo kuwa Uislamu haitakubaliwa kwake. Naye akhera atakuwa katika wenye hasara}. (Al Imran 85)
10.Ni kuipuuzia dini ya Allah hajifunzi dini wala kuyafanyia kazi maamrisho yake na dalili ni kauli ya Allah Mtukufu: {Na ni nani dhaalimu mkubwa kuliko yule anaye kumbushwa kwa Ishara za Mola wake Mlezi, kisha akazikataa? hakika Sisi tutajilipiza kwa wakosefu} (Sajdah 22). na maana ya kuipuuzia Dini: ni kuto kujifundisha yale yanayo paswa kuyajua katika dini katika yale ambayo ni wajibu katika dini kama kujifunza misingi ya dini kama itikadi na ibada.
Baada ya kutaja hayo ambayo yanabatilisha uislam inapendeze tukawazindua watu kuhusu mambo mawili muhimu nayo:
- Ni kwamba lengo la kutaja hivi vitenguzi nikutaka kuwakumbusha watu na kuwatahadharisha, hakika shetani na wasaidizi wake miongoni mwa watu wanao potosha dini na kuigeuza wanasubiri mapungufu kwa Waislamu ili watumie nafasi ya kughafilika kwao na ujinga wao ili wawatoe katika Dini ya haki na ili wawatowe katika njia ya pepo na kuwaelekeza kunako njia ya Motoni.
- Hivi vitenguzi vya uislam kuambatanisha na hali ya kimaisha ili kumpa hukumu kwamba huyu ni kafiri au sio kafiri ni katika majukumu ya wanachuoni wakubwa walio zama katika elimu, wao ndio wanao jua dalili na hukumu na sababu na vigezo vya kushuka hukumu mbalimbali kwa watu na sio kwa kila mtu anaweza kutoa hukumu hiyo.
Jawabu/ Sema: Haijuzu kumuhukukumu mtu kuwa ni wa Peponi au wa Motoni ispokuwa wale ambao dalili zimewaelezea kuwa ni watu wa Peponi, lakini kila mwenye kufanya wema inatarajiwa atapata thawabu na kwayule anaefanya maovu kupata adhabu na tunasema kwamba kila alie kufa akiwa na imani mafikio yake ni Peponi na kila mwwnye kufa katika ushirikina na ukafiri basi atakuwa katika watu wa Motoni, ubaya ulioje wa mafikio hayo.
Jawabu/ Sema: Hapana Muislam hahukumiwi kuwa kafiri kwa sababu ya maasi anayo yafanya hatakama ni madhambi makubwa midhali sio madhambi ambayo yanamfanya awe kafiri ambayo yameelezwa na sheria katika Qur'an na sunnahh na maswahaba hawakuelezea au maimamu wakubwa, Muislam anabaki kuwa Muumini na anakuwa ni katika wanao muasi Allah katika waislam walio tamka Shahada, mithali hajaingia katika madhambi yanayo muingiza katika ukafiri au shirki kubwa au unafiki mkubwa.
Jawabu/ Jambo la kutamka na ulimi ni jambo hatari sana kwa tamko moja tu mtu anaingia katika Uislam na mtu anaweza kutoka katika uislam kwa tamko moja tu na Allah atukinge na matamshi ya ulimi ambayo mtu anatamka bila kutarajia yana tofautiana miongoni mwake kuna maneno ya kikafiri ambayo yanayo batilisha Uislam na kuharibu ibada za mtu, kama vile kumtukana Mwenyezi Mungu na Mtume wake rehma na amani ziwe juu yake, au maneno ya kuwasifu watu wenye cheo na mawalii sifa za Mwenyezi Mungu na kuwaomba msaada na kunasibisha kwao mambo yote ya heri ambayo yanayopatikana kwa wanadamu na katika hayo ni kuwasifu sifa zilizo pindukia zinazo wanyanyua juu ya viumbe wengine na kuwaapia na kufanya masihara sheria ya Mwenyezi Mungu na hukumu zake, au kuchukia hukumu za Mwenyezi Mungu alizo shusha kwa waja wake, au kupinga hukumu zake alizo zipanga katika matukio yenye kuumiza katika mambo yasiyo pendeza katika mambo yanayo patikana katika dunia kama misiba katika mwili na mali na watoto na mengineyo
Miongoni mwa madhambi makubwa ambayo yanaharibu imani ya mtu na kuiharibu ni kusengenya na Kuteta tunatakiwa tuyatahadhari ukweli wa kutahadhari, tuhifadhi ndimi zetu kutokana na kila tamko ambalo linalo pingana na sheria ya Allah na sunnahh za Mtume wake rehma na amani ziwe juu yake, amesema Mtume rehma na amani ziwe juu yake: (Hakika mja anaweza kutamka neno moja linalo mridhisha Allah bila kulichukulia manani, ila Mwenyezi Mungu anamyanyua daraja kubwa na hakika mja anaweza kutamka neno katika maneno yanayo mchukiza Mwenyezi Mungu bila kulichukulia manani anamzamisha kwa sababu ya neno hilo katika Moto wa Jahanam). Imepokelewa na Imamu Bukhari.
Sema: Haikatiki ibada ya mja ila ni kwa kifo, dalili ni kauli ya Allah mtukifu: { Muabudu Mola wako mpaka kikufikie kifo} Hujirat99 na amesema Mtume rehma na amani ziwe juu yake kutoka kwa Athumani bin Madh'uni wakati alipo kufa: (Ama Othman Bin Madh'uni namuapa Allah amefikiwa na Umauti). Imetolewa na Imamu Bukhari, na kwakuwa Mtume rehma na amani ziwe juu yake hakuacha kufanya ibada katika maisha yake na maana ya yakini katika aya na hadithi hazina maana ya kufikia daraja ya juu katika Imani ambayo akifikia anaacha kufanya ibada kama wanavyo fasiri baadhi ya watu wanao potosha Dini ya Allah bali yakini inamaana ya kifo.
Jawabu/ Sema: Anaepangilia mambo ya mbinguni na ardhini na vilivyomo baina yake ni Mwenyezi Mungu peke yake hana mshirika hakuna mfalme asiekuwa Yeye wala hana mshirika wala msaidizi wala anae fanana nae utakasifu ni wake na ametukuka, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na yeye hakuwa na mamlaka yeyote juu yao, ila kwa sababu ya kuwajaribu tujue nani mwenye kuamini akhera na nani anaye tilia shaka. Na Mola wako Mlezi ni mwenye kuhifadhi kila kitu}. (Sabaa 22)
Jawabu/ Sema: Hakuna anaejua ghaibu ila ni Mwenyezi Mungu na hakuna anae fufua wafu ila ni Mwenyezi Mungu na ushahidi ni kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na lau kuwa ninayajua ya ghaibu ninge jizidishia mema mengi, wala ovu lisinge nigusa. Mimi si chochote ila ni mwonyaji na mbashiri kwa watu wanao amini} (Aaraf 188) akiwa Mtume rehma na amani zowe juu yake mbora wa viumbe hajuwi ghaibu nani asiekuwa yeye anae stahiki kujua elimu ya ghaibu.
Maimamu wanne ya kwamba yeyote mwenye kutegemea kuwa Mtume rehma na amani ziwe juu yake anajua ghaibu au anahuyisha mtu alie kufa, basi huyo atakuwa ametoka katika Uislamu, kwa kumkadhibisha Mwenyezi Mungu ambae alie muamrisha mtume wake aseme kuwambia wanadamu na majini: {Sema: Mimi sikwambiini kuwa ninazo hazina za Mwenyezi Mungu. Wala sijui mambo yaliyo fichikana. Wala sikwambiini kuwa mimi ni Malaika. Mimi sifuati ila yanayo funuliwa kwangu.} (Al-Anaam 50) na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Hakika kuijua Saa (ya Kiyama) kuko kwa Mwenyezi Mungu. Na Yeye ndiye anaye iteremsha mvua. Na anavijua viliomo ndani ya matumbo ya uzazi. Na haijui nafsi yeyote itachuma nini kesho. Wala nafsi yeyote haijui itafia nchi gani. Hakika Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kujua, Mwenye habari}. (Luqman 34), basi Mtume rehma na amani ziwe juu yake hajui katika elimu ya ghaibu ila yale ambayo aliyo funuliwa Mwenyezi Mungu kwake na akamfundisha na Mtume rehma na amani ziwe juu yake hakuwahi kujidai katika uhai wake hata siku moja kuwa alimuhuyisha yeyote katika maswahaba zake au yeyote katika watoto wake ambao walio kufa kabla yake, hayo yote Mtume hakuyaweza vipi kwa asiekuwa Mtume rehma na amani ziwe juu yake.
Jawabu/ Sema: Kila Muislamu Muumini mchamungu basi mtu huyo kwa Allah ni walii, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Jueni kuwa vipenzi vya Mwenyezi Mungu hawatakuwa na hofu wala hawatahuzunika (62) Hao ni ambao wameamini na wakawa wanamcha Mungu} (Yunus 62-63) Uwalii sio maalumu kwa baadhi ya waislam, ispokua daraja za uwalii unatofautiana na Maana ya uchamungu: Ni kufanya yale aliyo amrisha Mwenyezi Mungu na Mtume wake rehma na amani ziwe juu yake na kujiepusha na yale aliyo yakataza Mwenyezi Mungu na Mtume wake rehma na amani ziwe juu yake na kila muumini uwalii wake ni kwakulingana na kiasi cha uchamungu wake na utekelezaji wake wa ibada.
Jawabu/ Sema: atakae kuwa walii katika watu wasiokuwa mitume hakika watu hao hawaja takasika na kufanya madhambi makubwa au madogo, hakika wamewahi kuingia katika madhambi wengi katika mawalii wakubwa wa Mwenyezi Mungu wakakosea na kutenda dhambi lakini walifanya haraka kutubia dhambi zao na kuomba msamaha na wakasamehewa na Mwenyezi Mungu.
Jawabu/ Sema: Sahihi ni kwamba hidhri ni Mtume katika mitume wa Mwenyezi Mungu alikufa kabla ya kuzaliwa Mtume muhammad rehma na amami ziwe juu yake, kwasababu Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: {Nasi hatukumjaalia mwanaadamu yeyote kabla yako kuwa na maisha ya milele. Basi je! Ukifa wewe, wao wataishi milele?} (Anbiyaa 34). Laiti angekuwa hai angemfuata Mtume Muhammad rehma na amani ziwe juu yake na angepigana jihadi na yeye kwasababu Mtume Muhammad rehma na amani ziwe juu yake ametumwa kwa watu wote na majini wote, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Sema: Enyi watu! Hakika mimi ni Mtume kwenu nyinyi nyote} (Al-Aarafi 158). Na Mtume Muhammad rehma na amani ziwe juu yale alisema: (Hakika nimeonyeshwa katika usiku wenu huu kwamba hakuna kichwa) Imepokelewa na Imamu Bukhari, na hii ni dalili tosha kuwa Hidhri alisha kufa katika wafu na kwakuwa alisha kufa hasikii wito wa yeyote atakae mwita wala hawezi kumuongoa alie potea kunako njia ya haki pindi atakapo muomba amuongoze na visa vinavyo tajwa kuhusu kukutana na baadhi ya watu na visa vya kuonekana kwake na kukaa na baadhi ya watu, hakika visa hivyo ni ndoto na uwongo ulio wazi haumpotezi yule alie pewa na Mwenyezi Mungu elimu akili na busara.
Jawabu/ Sema: Walio kufa hawasikii kwa kauli ya Mwenyezi Mungu: {Hukuwa wewe nimwenye kuwafanya wasikie walioko makaburini} (Faatwir 22) na amesema Mwenyezi Mungi mtukifu: {Kwa hakika wewe huwezi kuwafanya maiti wasikie}. (Namli 80) na maiti hawawezi kumjibu kwa mwenye kuwaomba, Amesema Mwenyezi Mungu: { Na hao mnao waomba badala yake hawamiliki hata ugozi wa kokwa ya tende (13) Mkiwaomba hawasikii maombi yenu; na hata wakisikia hawakujibuni. Na siku ya kiyama watakataa ushirikina wenu. Na hapana atakaye kupa habari vilivyo kama Yeye Mwenye habari} ( Fatwir 13-14) na kauli ya Mwenyezi Mungu: {Na nani mpotofu mkubwa kuliko hao wanao waomba, badala ya Mwenyezi Mungu, ambao hawatawaitikia mpaka Siku ya Kiyama na wala hawatambui maombi yao} (Ahkaf 5).