Skip to content

Utakapo ulizwa: Je, inajuzu kuomba hifadhi kwa asiekuwa Mwenyezi Mungu?

السؤال

Sawali/ Utakapo ulizwa: Je, inajuzu kuomba hifadhi kwa asiekuwa Mwenyezi Mungu?

الجواب

Jawabu/ Sema: linakuwa wazi jawabu kwa kujua aina tatu za kuomba msaada nazo:

  1. Kuomba hifadhi kwa kumpwekesha Mwenyezi Mungu kwa kufanya ibada: nako ni kumuomba hifadhi Mwenyezi Mungu kutokana na kila unacho kiogopa. amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Sema: Najikinga kwa Mola Mlezi wa mapambazuko, (1) Na shari ya alivyo viumba, (2)} (Falaqi 1-2) na anasema Mwenyezi Mungu:Sema: Ninajikinga kwa Mola Mlezi wa wanaadamu, (1) Mfalme wa wanaadamu (2) Mungu wa wanaadamu (3) Na shari ya wasiwasi wa Shetani, Khannas}. (Al Nnasi 1-4)
  2. Ni kuomba hifadhi kwa njia ya halali: nako nikuomba hifadhi kwa viumbe walio hai waliopo na wenye uwezo kukusaidia jambo ulilo waomba na katika yale mambo ambayo yanawezekana kisheria, anasema Mtume rehma na amani ziwe juu yake: Mwenyekupata makimbilio au hifadhi basi na akimbilie huko) Imepokelewa na Imamu Muslim.

3-Kuomba hifadhi kwa njia ya ushirikina: nako ni kukiomba hifadhi kisichokuwa Mwenyezi Mungu katika mambo ambayo hakuna anae yaweza ila ni Mwenyezi Mungu, amesema Mwenyezi Mungu: {Na hakika walikuwako wanaume katika watu walio kuwa wakitafuta kujikinga kwa wanaume wa kijini; kwa hivyo wakawazidisha madhambi} Jinni 6