Skip to content

ukiulizwa: je maiti katika Mawalii na wengineo wanawajibu walio hai kwa aliyeomba nusra na msaada kwao?

السؤال

Swali/ ukiulizwa: je maiti katika Mawalii na wengineo wanawajibu walio hai kwa aliyeomba nusra na msaada kwao?

الجواب

Jawabu/ sema: wao hawajibu mwenye kuwaita na hawawezi kujibu mwenye kuwaomba au akawaomba nusra, amesema Mwenyezi Mungu: {Na hao mnao waomba badala yake hawamiliki hata ugozi wa kokwa ya tende (13) Mkiwaomba hawasikii maombi yenu; na hata wakisikia hawakujibuni. Na Siku ya Kiyama watakataa ushirikina wenu} (Fatwir 13-14). Hasara ilioje kwa mtu alie danganywa na mashetani na walinganizi wanao potosha waliwapambia ibada za kuwaomba maiti na watu walio zikwa, wakiwemo manabii mawalii na watu wema, amesema Mwenyezi Mungu:{Na nani mpotofu mkubwa kuliko hao wanao waomba, badala ya Mwenyezi Mungu, ambao hawatawaitikia mpaka Siku ya Kiyama na wala hawatambui maombi yao} (Ahqaaf 5).