Skip to content

Utakapo ulizwa: Ni ipi Hukumu ya kukiapia kisichokua Mwenyezi Munguu Mtukufu?

السؤال

Swali/ Utakapo ulizwa: Ni ipi Hukumu ya kukiapia kisichokua Mwenyezi Munguu Mtukufu?

الجواب

Jawabu/ Sema: Haijuzu kukiapia kisichokua Mwenyezi Mungu Mtukufu, Amesema Mtume rehma na amani ziwe juu yake: (Atakae kuwa ni mwenye kuapa basi aapie kwa jina la Mwenyezi Mungu) Imepokelewa na Bukhari. Mtume rehma na amani ziwe juu yake alikataza kuapia kisichokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, kama ilivyo kuja katika kauli ya mtume rehma na amani ziwe juu yake: (Msiapie kwa majina ya wazazi wenu wala kwa majina ya Matwaghuti) Imepokelewa na Muslim na Matwaghuti: -ni kila kinacho abudiwa kinyume cha Allah, kikiwa kimeridhia au kiongozi asie fuata sheria za Allah au sheria zozote zisizokuwa za Allah- bali mtume rehma na amni ziwe juu yake alijalia kufanya hivyo ni katika shirki, kama ilivyo katika kauli yake Mtume rehma na amani ziwe juu yake: (Mwenye kukiapia kisichokuwa Mwenyezi Mungu atakuwa amekufuru au amemshirikisha Mwenyezi Mungu) na amesema Mwenyezi Mungu: (Mwenyekuapia kwa uaminifu wake atakuwa sio katika sisi) Imepokelewa na Imamu Ahmad na Ibn Hibani ma Hakim kwa upokezi sahihi.

Muislam ajitahadhari na kuapia kwa jina la Mtume au walii, au kuapia kwa cheo amana na Alkaaba,na mengineyo katika viumbe vya Mwenyezi Mungu.