utakapo ulizwa: je, inajuzu kuomba nusra kinyume na Mwenyezi Mungu katika yale ambayo hakuna anaeyaweza ila ni Mwenyezi Mungu katika mambo yanayo leta heri au kuzuia shari?
السؤال
Swali/ utakapo ulizwa: je, inajuzu kuomba nusra kinyume na Mwenyezi Mungu katika yale ambayo hakuna anaeyaweza ila ni Mwenyezi Mungu katika mambo yanayo leta heri au kuzuia shari?
الجواب
Jawabu/ Sema: kufanya hivyo nikatika ushirikina mkubwa unao tengua matendo ya mwanadamu na unao mtuoa mtu katika dini na kumfanya aishi milele katika moto kwa yule atakae ufanya na hakutubia kabla ya kufa, kwa kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Nani yule anaye mjibu mwenye shida pale anapo mwomba na akaiondoa dhiki} (Namli 62) Maana yake ni kwamba hakuna mwenye uwezo wa kumjibu ila ni Mwenyezi Mungu na hakuna mwenye kuondosha madhara ila ni Mwenyezi Mungu. akawakamea Mwenyezi Mungu kila mwenye kuomba nusra kwa asie kuwa yeye kwa kuanza maneno yake kwa kuuliza, kwa sababu kuomba nusra ni kufanya ibada vilevile kuomba msaada, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Kumbukeni wakati mkiomba nusra kwa Mola wenu mlezi} (Anfal 9) na imethibiti katika sahihi bukhari kutoka kwa Abuu Hurayrah radhi za Allah ziwe juu yake kwamba hakika Mtume rehma za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake alisema: nisimkute mmoja wenu atakae kuja siku ya Kiyama akiwa na ngamia anaetoa sauti ya juu, kisha akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu niokoe na ninusuru, ispokuwa nitasema: tayari nimesha kufikishia hakika mimi similiki chochote katika hilo unalo niomba, nisimkute mmoja wenu anakuja siku ya qiyama akiwa na farasi anaetoa sauti ya chini, kisha anasema: ewe mtume niokowe, nitasema similiki chochote kwa Mwenyezi Mungu nimesha kufikishia, Imepokelewa na Bukhari na Muslim. na ijulikane wazi kuwa inajuzu kuomba nusra kwa wanadamu walio hai ambao tunawaona, sio wale ambao hawapo ikiwa ni katika mambo anayo na uwezo nayo na kuomba nusra kwa mwanadamu allie hai ina maana ya kumuomba msaada, katika yale anayo yaweza kiumbe, kama alivyo omba rafiki wa mussa kwa mussa amsaidie kutokana na adui yao, amesema Allah Mtukufu: {Yule mwenzake alimtaka msaada kumpiga adui yake} (Qaswaswi15) ama kuomba nusra kwa wasiokuwepo miongoni mwa watu na majini na watu wa makaburini wanachuoni wamekubaliana kuwa niharam na nibatili na nikatika Ushirikina.