utakapo ulizwa: je inajuzu kumuabudia kwa majina ya asiekuwa Mwenyezi Mungu kama vile mja wa Nabii au mja wa Hussain na mfano wake?
السؤال
Swali/ utakapo ulizwa: je inajuzu kumuabudia kwa majina ya asiekuwa Mwenyezi Mungu kama vile mja wa Nabii au mja wa Hussain na mfano wake?
الجواب
Jawabu/ sema: Haijuzu kwani wanachuoni wamekubaliana juu ya uharamu wa kila jina linalo abudiwa kinyume cha Mwenyezi Mungu na ni wajibu kubadilisha jina linalo abudiwa kinyume cha Mwenyezi Mungu, kama jina: Mja wa Nabii, mja wa Mtume, mja wa Hussein na mja wa Al Kaaba na majina mengine mfano wa majina hayo na majina bora na yanayo pendeza kwa Mwenyezi Mungu ni: (Abdullah na Abdurahmani) kama ilivyo kuja katika hadithi sahihi kutoka kwa Mtume rehma na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: (Hakika majina yanayo pendeza zaidi kwa Mwenyezi Mungu ni Abdullah na Abdurahmani) Imepokelewa na Imamu Muslim. ni wajubu kubadilisha majina yanayo abudiwa kinyume na Mwenyezi Mungu na hii ni kwa wale waliopewa majina hayo na wapo hai walio itwa majina yanayo abudiwa kinyume cha Mwenyezi Mungu.