Utakapo ulizwa: inajuzu kutabaruku kwenye Miti au Mawe au Michanga?
السؤال
Swali/ Utakapo ulizwa: inajuzu kutabaruku kwenye Miti au Mawe au Michanga?
الجواب
Jawabu/ Jawabu: Kufanya hivyo nikatika Ushirikina, imepokelewa kutoka kwa Imamu Ahmad na Tirmidhiy kutoka kwa Abi Waaqid Allaythiy alisema: Tulitoka pamoja na Mtume rehma na amani ziwe juu yake kwenda khunayni na sisi tukiwa ni waislam wapya na washirikina walikuwa na Mti wa Mkunazi wakiketi chini yake kwa ajili ya kuomba na kutundika silaha zao, Mti huo unaitwa dhatu anwat (Mti wanao tundika juu yake Silaha zao) mara tukapita kwenye Mti wa Mkunazi mwingine tukamwambia Mtume -rehma na amani ziwe juu yake- akawajibu Mtume -rehma na amani ziwe juu yake-: (Allah ni Mkubwa hakika hilo mlilo sema ni mwenendo wa watu wajinga walio pita, nina muapa Allah ambae nafsi yangu iko mikononi mwake, hayo mliyosema ni sawa na yale waliyo sema wana wa Izrael kumwambia Mussa: {Tuwekee waungu tuwaabudu kama makafiri walivyo na miungu, Musa akasema hakika nyinyi ni watu wajinga} (A'araf 138) mtazidi kufuata myenendo ya watu waliokuwa kabla yenu).