Utakapo ulizwa: ni ipi Hukumu ya kukiwekea nadhiri kisichokuwa Mwenyezi Munguu Mtukufu.
السؤال
Swali/ Utakapo ulizwa: ni ipi Hukumu ya kukiwekea nadhiri kisichokuwa Mwenyezi Munguu Mtukufu.
الجواب
Jawabu/ Sema: kufanya hivyo ni shiriki kubwa kwa kauli Mtume rehma na amani ziwe juu yake: (Mwenye kuweka nadhiri ya kumtii Mwenyezi Mungu basi amtii na mwenye kuweka nadhri ya kumuasi Mwenyezi Mungu basi asimuasi) Imepokelewa na imamu Bukhari, nadhiri ni ibada ya kusema na ya kutoa mali au ya kutoa mali au ya kimwili, kulingana na kile alicho kiweka nadhiri na maana ya nadhiri: ni kujilazimisha kufanya jambo ambalo sio lazima kwake kisheria, kwa kutarajia kupata anacho kitarajia au kukinga ambacho ambacho hapendi kimpate, au kwa kushukuru neema iliyo mshukia au janga lililo muondokea nadhiri ni katika ibada ambazo hazijuzu kumfanyia yeyote kinyume cha Mwenyezi Mungu kwasababu Mwenzi mungu amewasifu wenye kutekeleza nadhiri, akasema Mwenyezi Mungu: {Wanatimiza ahadi,na wanaiogopa siku ambayo shari yake inaenea sana} (insan 7)
Na kuna kanuni inasema: kila kitendo ambacho amesifiwa na Mwenyezi Mungu mwenye kukitenda basi kimo katika ibada, kile ambacho ni ibada kumfanyia asiekuwa Mwenyezi Mungu ni Ushirikina.