Skip to content

Kusema kwangu: Sub-haanallaah, na Alhamdulillaah, na Laa ilaaha illa llaah, na Allaahu Akbaru, kunapendeka sana kwangu kuliko vitu vyote vilizochomozewa na jua

Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-:

"Kusema kwangu: Sub-haanallaah, na Alhamdulillaah, na Laa ilaaha illa llaah, na Allaahu Akbaru, kunapendeka sana kwangu kuliko vitu vyote vilizochomozewa na jua".

«لَأَنْ أَقُولَ: سُبْحَانَ اللهِ، وَالْحَمْدُ لِلهِ، وَلَا إِلَهَ إِلَّا اللهُ، وَاللهُ أَكْبَرُ، أَحَبُّ إِلَيَّ مِمَّا طَلَعَتْ عَلَيْهِ الشَّمْسُ».

Imepokelewa Imamu Muslim
Sahihi
Ufafanuzi

Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa kumtaja Allah Mtukufu kwa maneno haya matukufu ni bora kuliko dunia na vilivyomo, na utajo huo ni kusema: "Sub-haana llaah": Ni kumtakasa Mwenyezi Mungu kutokana na mapungufu. "Alhamdulillaah": Ni kumsifia kwa sifa za ukamilifu pamoja na kumpenda na kumtukuza. "Laa ilaaha illa llaah": Hakuna muabudiwa wa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu. "Allaahu Akbaru: Mkubwa na Mtukufu kuliko kila kitu.

Maana ya Maneno

...:

Katika Faida za Hadithi

Himizo la kumtaja Mwenyezi Mungu, nakuwa hilo linapendeka zaidi kuliko vyote vilivyochomozewa na jua.

Himizo la kukithirisha dhikiri; kwakuwa ndani yake kuna malipo na fadhila kubwa.

Starehe za dunia ni ndogo na matamanio yake ni yenye kuondoka.

Rejea

Swahiih Muslim (4/ 2072) (2695).

Zaidi (8)

بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين.

لسليم الهلالي (2/ 496).

شرح رياض الصالحين.

لابن عثيمين (5/ 485).

نزهة المتقين شرح رياض الصالحين.

لمصطفى الخِن وغيره (2/ 970).

تطريز رياض الصالحين.

لفيصل آل المبارك (ص772).