“Hakuna Muislamu anayetawadha na akautia vizuri udhu wake, kisha akasimama na kuswali rakaa mbili, akielekea kwa moyo wake na uso wake ndani ya rakaa hizo, isipokuwa Pepo itastahiki kwake.”
Kutoka kwa Uqba bin Amir, Mwenyezi Mungu amuwie radhi, amesema: “Tulikuwa na zamu ya kuchunga ngamia, basi ikafika zamu yangu nikawapeleka jioni, nikamkuta Mtume rehema na amni ziwe juu yake akiwa amesimama akiwahadithia watu, nikamkuta akiwa katika kauli yake:
“Hakuna Muislamu anayetawadha na akautia vizuri udhu wake, kisha akasimama na kuswali rakaa mbili, akielekea kwa moyo wake na uso wake ndani ya rakaa hizo, isipokuwa Pepo itastahiki kwake.” Akasema, nikasema: Ni kheri iliyoje hii, mara ghafla nikasikia msemaji mmoja mbele yangu akisema: Ile ya kabla yake ndio ilikuwa bora, basi nikatazama, mara nikamuona ni Omari, akasema: Nimekuona umekuja hivi karibuni, akasema: “Hakuna yeyote kati yenu atakayetawadha vizuri - au akaukamilisha vizuri- kisha akasema: Nashuhudia ya kwamba hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, na kwamba Muhammad ni mja wa Mwenyezi Mungu na Mtume wake, isipokuwa atafunguliwa milango minane ya Pepo, aingie mlango wowote autakao".
«مَا مِنْ مُسْلِمٍ يَتَوَضَّأُ فَيُحْسِنُ وُضُوءَهُ، ثُمَّ يَقُومُ فَيُصَلِّي رَكْعَتَيْنِ، مُقْبِلٌ عَلَيْهِمَا بِقَلْبِهِ وَوَجْهِهِ، إِلَّا وَجَبَتْ لَهُ الْجَنَّةُ» قَالَ فَقُلْتُ: مَا أَجْوَدَ هَذِهِ، فَإِذَا قَائِلٌ بَيْنَ يَدَيَّ يَقُولُ: الَّتِي قَبْلَهَا أَجْوَدُ، فَنَظَرْتُ فَإِذَا عُمَرُ قَالَ: إِنِّي قَدْ رَأَيْتُكَ جِئْتَ آنِفًا، قَالَ: «مَا مِنْكُمْ مِنْ أَحَدٍ يَتَوَضَّأُ فَيُبْلِغُ - أَوْ فَيُسْبِغُ - الْوَضُوءَ ثُمَّ يَقُولُ: أَشْهَدُ أَنْ لَا إِلَهَ إِلَّا اللهُ وَأَنَّ مُحَمَّدًا عَبْدُ اللهِ وَرَسُولُهُ إِلَّا فُتِحَتْ لَهُ أَبْوَابُ الْجَنَّةِ الثَّمَانِيَةُ يَدْخُلُ مِنْ أَيِّهَا شَاءَ».
Alibainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake wakati akiwaeleza watu fadhila mbili kubwa: Ya kwanza: Mwenye kutawadha vizuri, akaupendezesha vizuri udhu, na akaukamilisha, na akaukamilisha katika namna ilivyoelekezwa, na akakipa kila kiungo haki yake katika maji, kisha akasema: Nashuhudia ya kwamba hakuna mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, na kwamba Muhammad ni mja wa Mwenyezi Mungu na Mtume wake; Isipokuwa atafunguliwa milango minane ya Peponi, aingie mlango autakao. Pili: Mwenye kutawadha udhu huu kamili, kisha akasimama baada ya udhuu huu na kuswali rakaa mbili; Akiwa ameelekea ndani ya swala kwa moyo wake, kwa ikhlaswi na utulivu, na akanyenyekeza uso wake na viungo vyote vya mwili wake kwa Mwenyezi Mungu, isipokuwa Pepo itakuwa ni wajibu kwake.
Ukubwa wa fadhila za Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa kumpa malipo makubwa kwa amali ndogo.
Sheria ya kueneza maji ya udhu na kutawadha kwa ukamilifu, na kuswali rakaa mbili kwa unyenyekevu baada yake, na malipo makubwa yanayopatikana kwayo.
Kueneza maji ya udhu, na kuleta dua hii baada yake, ni katika sababu za kuingia peponi.
Sunna ya kusema dhikiri hii kwa mwenye kuoga pia.
Maswahaba walikuwa na shauku ya kufanya mema, kama vile kujifunza na kusambaza elimu, na ushirikiano wao katika kufanya hivyo na katika masuala ya riziki zao.
Dhikri baada ya kutawadha huutakasa moyo na kuusafisha na ushirikina, kama vile udhuu unavyousafisha mwili na kuuondoa uchafu.
Swahiih Muslim (1/ 209) (234).
Zaidi (4)
توضيح الأحكام.
للبسام (1/ 251).
المنهاج شرح صحيح مسلم بن الحجاج.
للنووي (3/ 120).
Imenukuliwa katika vitabu
11 Vitabu- YALIYO CHAGULIWA KUTOKA KATIKA SOKO LENYE FAIDA KATIKA THAWABU ZA MATENDO MEMA.المنتقى من المتجر الرابح في ثواب العمل الصالح"Hakuna yeyote atakaye tawadha vizuri kisha akasema( Ash-hadu an laailaha ilallah wa anna Muhamada Rasulallah) Isipokuwa atafunguliwa milango minane ya pepo, ili aingie katika mlango aupendao"
- YALIYO CHAGULIWA KUTOKA KATIKA SOKO LENYE FAIDA KATIKA THAWABU ZA MATENDO MEMA.المنتقى من المتجر الرابح في ثواب العمل الصالح"Hakuna muislamu yeyote atakaye tawadha akaufanya vizuri udhu wake, kisha akasimama akaswali rakaa mbili, akinyenyekea ndani ya swala hiyo kwa moyo wake na mwili wake, isipokuwa atastahiki kuingia peponi"
Zaidi (9)
- الأربعون في تعظيم قدر الصلاةالأربعون في تعظيم قدر الصلاة «مَا مِنْ مُسْلِمٍ يَتَوَضَّأُ فَيُحْسِنُ وُضُوءَهُ، ثُمَّ يَقُومُ فَيُصَلِّي رَكْـــــــعَتَيْنِ، مُقْبِلٌ عَلَيْهِمَا بِقَلْبِهِ وَوَجْــــهِهِ، إِلَّا وَجَبَتْ لَهُ الْجَنَّةُ».
- الخطب المنبرية موسوعة الخطب المنبرية (القسم الثاني)«مَا مِنْ مُسْلِمٍ يَتَوَضَّأُ فَيُحْسِنُ وُضُوءَهُ، ثُمَّ يَقُومُ فَيُصَلِّي رَكْعَتَيْنِ، مُقْبِلًا عَلَيْهِمَا بِقَلْبِهِ وَوَجْهِهِ، إِلَّا وَجَبَتْ لَهُ الجَنَّةُ»
- الذكر والدعاء والعلاج بالرقي من الكتاب والسنة"ما منكم من أحد يتوضأ فيسبغ الوضوء ثم يقول: "أشهد أن لا إله إلا الله وحده لا شريك له، وأشهد أن محمدًا عبده ورسوله: إلا فتحت له أبواب الجنة الثمانية يدخل من أيها شاء" .
- خطب تعظيم قدر الصلاة"مَا مِنْ مُسْلِمٍ يَتَوَضَّأُ فَيُحْسِنُ وُضُوءَهُ، ثُمَّ يَقُومُ فَيُصَلِّي رَكْعَتَيْنِ، مُقْبِلٌ عَلَيْهِمَا بِقَلْبِهِ وَوَجْهِهِ، إِلَّا وَجَبَتْ لَهُ الْجَنَّةُ"
- مجموعة زاد التربية الإسلامية (1)، والسيرة النبوبة (1)، والعقيدة (1)، والفقه (1)مجموعة زاد الفقه (1)«مَا مِنْكُمْ مِنْ أَحَدٍ يَتَوَضَّأُ فَيُسْبِغُ الْوَضُوءَ ثُمَّ يَقُولُ: أَشْهَدُ أَنْ لَا إِلَهَ إِلَّا اﷲُ وَأَنَّ مُحَمَّداً عَبْدُ اﷲِ وَرَسُولُهُ إِلَّا فُتِحَتْ لَهُ أَبْوَابُ الْجَنَّةِ الثَّمَانِيَةُ يَدْخُلُ مِنْ أَيِّهَا شَاءَ»
- مشروع منهاج زادكزادك 1 طالب«مَا مِنْكُمْ مِنْ أَحَدٍ يَتَوَضَّأُ فَيُبْلِغُ أَوْ فَيُسْبِغُ الْوَضُوءَ، ثُمَّ يَقُولُ: أَشْهَدُ أَن لَا إِلَهَ إِلاَ اللهُ وأَنَّ مُحَمَّدًا عَبْدُ اللهِ ورَسُولُهُ، إِلَّا فُتِحَتْ لَهُ أَبْوَابُ الْجَنَّةِ الثَّمَانِيَةُ يَدْخُلُ مِن
- من الأحكام الفقهية في الطهارة والصلاة والجنائز«مَا مِنْكُمْ مِنْ أَحَدٍ يَتَوَضَّأُ فَيُسْبِغُ الْوَضُوءَ، ثُمَّ يَقُولُ: أَشْهَدُ أَنْ لَا إِلَهَ إِلَّا اللهُ وَأَنَّ مُحَمَّدًا عَبْدُ اللهِ وَرَسُولُهُ إِلَّا فُتِحَتْ لَهُ أَبْوَابُ الْجَنَّةِ الثَّمَانِيَةُ يَدْخُلُ مِنْ أَيِّهَ
- نبراس طالب (1)1(أَشْهَدُ أَنْ لَا إِلَهَ إِلَّا الله وأَنَّ مُحَمَّدًا عَبْدُ اللهِ وَرَسُولُهُ).
- نبراس طالب (1)1«مَا مِنْكُمْ مِنْ أَحَدٍ يَتَوَضَّأُ فَيُبْلِغُ أَوْ فَيُسْبِغُ الْوَضُوءَ، ثُمَّ يَقُولُ: أَشْهَدُ أَلَّا إِلَهَ إِلاَ اللهُ وأَنَّ مُحَمَّدًا عَبْدُ اللهِ ورَسُولُهُ، إِلَّا فُتِحَتْ لَهُ أَبْوَابُ الْجَنَّةِ الثَّمَانِيَةُ يَدْخُلُ مِنْ