Siku moja mtu mmoja alikuwa akipita njiani akakuta tawi la miba likiwa njiani akaliondosha, Allah akamshukuru na akamfutia madhambi yake
Kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake ya kwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema:
"Siku moja mtu mmoja alikuwa akipita njiani akakuta tawi la miba likiwa njiani akaliondosha, Allah akamshukuru na akamfutia madhambi yake".
«بَيْنَمَا رَجُلٌ يَمْشِي بِطَرِيقٍ وَجَدَ غُصْنَ شَوْكٍ عَلَى الطَّرِيقِ فَأَخَّرَهُ، فَشَكَرَ اللَّهُ لَهُ فَغَفَرَ لَهُ».
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kwamba siku moja kuna mtu mmoja alikuwa akitembea njiani akapita katika tawi mti wa miba likiwa barabarani likiwaudhi waislamu, akalivuta na akaliondosha njiani, basi Mwenyezi Mungu akamshukuru na akamsamehe.
Fadhila za kuondoa udhia njiani, na kwamba hilo ni sababu ya kuupata msamaha wa Mwenyezi Mungu.
Kutodharau matendo mema hata yakiwa ni madogo.
Uislamu ni dini ya usafi na kulinda mazingira na amani ya jamii nzima.
Swahiih Al Bukhaariy (1/ 132) (652).
Swahiih Muslim (3/ 1521) (1914).
Zaidi (6)
نزهة المتقين شرح رياض الصالحين.
لمجموعة من الباحثين (1/ 156).
شرح رياض الصالحين.
لابن عثيمين (2/ 175).
بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين.
لسليم الهلالي (1/ 207).