Skip to content

Mmbora wenu ni yule aliyejifunza Qur'ani na akaifundisha

Imepokewa kutoka kwa Othman -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema:

"Mmbora wenu ni yule aliyejifunza Qur'ani na akaifundisha".

«خَيْرُكُمْ مَنْ تَعَلَّمَ الْقُرْآنَ وَعَلَّمَهُ».

Imepokelewa na Al-Bukhaariy
Sahihi
Ufafanuzi

Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa muislamu bora na aliye na daraja ya juu zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu: Ni yule aliyejifunza Qur'ani, kwa kuisoma na kuihifadhi na kuisoma vizuri na kuielewa na kuitafsiri, na akamfundisha mwingine kile alichonacho katika elimu za Qur'ani pamoja na kuifanyia kazi.

Katika Faida za Hadithi

Kumebainishwa utukufu wa Qur'ani, nakuwa ndio maneno bora; kwani ni maneno ya Allah.

Mwanafunzi bora ni yule anayefundisha wengine, hatosheki kujifunza mwenyewe pekee.

Kujifunza Qur'ani na kuifundisha kunakusanya, kuisoma na maana yake na hukumu zake.

Rejea

Swahiih Al Bukhaariy (6/ 192) (5027).

Zaidi (8)

فتح الباري شرح صحيح البخاري.

لابن حجر العسقلاني (1/ 374).

بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين.

لسليم الهلالي (2/ 226).

نزهة المتقين شرح رياض الصالحين.

لمصطفى الخن وغيره (1/ 740).

شرح رياض الصالحين.

لابن عثيمين (4/ 638).