Skip to content

Adh-kari za baada ya sala ya faradhi hapati hasara msomaji au mfanyaji wake, kusema Sub-haana llahi mara thelathini na tatu (33), Al-hamdulillahi mara thelethini na tatu (33), Allahu Akbaru mara thelathini na nne (34)

Kutoka kwa Ka'b Bin Ujrah Radhi za Allah ziwe juu yake kutoka kwa Mtume rehema na amani za Allah ziwe juu yake alisema:

"Adh-kari za baada ya sala ya faradhi hapati hasara msomaji au mfanyaji wake, kusema Sub-haana llahi mara thelathini na tatu (33), Al-hamdulillahi mara thelethini na tatu (33), Allahu Akbaru mara thelathini na nne (34)".

«مُعَقِّبَاتٌ لَا يَخِيبُ قَائِلُهُنَّ -أَوْ فَاعِلُهُنَّ- دُبُرَ كُلِّ صَلَاةٍ مَكْتُوبَةٍ، ثَلَاثٌ وَثَلَاثُونَ تَسْبِيحَةً، وَثَلَاثٌ وَثَلَاثُونَ تَحْمِيدَةً، وَأَرْبَعٌ وَثَلَاثُونَ تَكْبِيرَةً».

Imepokelewa Imamu Muslim
Sahihi
Ufafanuzi

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuhusu Adhkari (Dua) hatopata hasara wala kujuta msemaji wake, bali maneno haya yanathawabu, na yanakuja kwa kufuatana, na husemwa baada ya swala za faradhi, nayo ni: "Sub-haana llaah" -Ametakasika Mwenyezi Mungu- mara thelathini na tatu, yaani ametakasika Mtukufu na kila mapungufu. "Na Alhamdulillaah" Mara thelathini na tatu, nako ni kumsifu Mwenyezi Mungu kwa ukamilifu uliotimia pamoja na kumpenda na kumtukuza. "Allaahu Akbaru" Mara thelathini na nne, Mwenyezi Mungu ni mkubwa mno na ni Mtukufu na Mwenye nguvu kuliko kila kitu.

Maana ya Maneno

...:

Katika Faida za Hadithi

Fadhila za kusema Sub-haanallaah, na Alhamdulillaah, na Allaahu Akbar, maneno haya ndio mema yenye kubakia.

Rejea

Swahiih Muslim (1/ 418) (596).

Zaidi (10)

بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين.

لسليم الهلالي (2/ 501).

نزهة المتقين شرح رياض الصالحين.

لمجموعة من الباحثين (2/ 976).

مرقاة المفاتيح شرح مشكاة المصابيح.

لعلي القاري (2/ 766).

تيسير العلام.

للبسام (ص227).

فيض القدير شرح الجامع الصغير.

لزين الدين المناوي (5/ 525).