Hakuna Muislamu yeyote atakayefikwa na msiba akasema aliyoamrishwa na Mwenyezi Mungu: "Innaa lillaahi wa innaa ilaihi raajiuun" (Hakika sisi sote ni wa Mwenyezi Mungu na hakika sisi sote kwake tutarejea) [Baqara: 156], Ewe Mwenyezi Mungu nilipe katika msiba wangu, na unipe badala bora kuliko hili, isipokuwa Mwenyezi Mungu atampa badala bora kuliko hiyo
Kutoka kwa Ummu Salama radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume rehema na amani za Allah ziwe juu yake akisema:
"Hakuna Muislamu yeyote atakayefikwa na msiba akasema aliyoamrishwa na Mwenyezi Mungu: "Innaa lillaahi wa innaa ilaihi raajiuun" (Hakika sisi sote ni wa Mwenyezi Mungu na hakika sisi sote kwake tutarejea) [Baqara: 156], Ewe Mwenyezi Mungu nilipe katika msiba wangu, na unipe badala bora kuliko hili, isipokuwa Mwenyezi Mungu atampa badala bora kuliko hiyo" Akasema: Alipofariki Abuu Salama, nikasema: Ni Muislamu gani atakuwa bora kuliko Abuu Salama? Nyumba ya kwanza aliyohamia Mtume rehema na amani ziwe juu yake, kisha mimi nikasema maneno hayo, Mwenyezi Mungu akanipa mbadala wake ambaye ni Mtume rehema na amani ziwe juu yake.
«مَا مِنْ مُسْلِمٍ تُصِيبُهُ مُصِيبَةٌ فَيَقُولُ مَا أَمَرَهُ اللهُ: {إِنَّا لِلهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ} [البقرة: 156]، اللَّهُمَّ أْجُرْنِي فِي مُصِيبَتِي، وَأَخْلِفْ لِي خَيْرًا مِنْهَا، إِلَّا أَخْلَفَ اللهُ لَهُ خَيْرًا مِنْهَا»، قَالَتْ: فَلَمَّا مَاتَ أَبُو سَلَمَةَ قُلْتُ: أَيُّ الْمُسْلِمِينَ خَيْرٌ مِنْ أَبِي سَلَمَةَ؟ أَوَّلُ بَيْتٍ هَاجَرَ إِلَى رَسُولِ اللهِ صلى الله عليه وسلم، ثُمَّ إِنِّي قُلْتُهَا، فَأَخْلَفَ اللهُ لِي رَسُولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم.
Ameeleza mama wa waumini Ummu Salama radhi za Allah ziwe juu yake ya kwamba yeye alimsikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake akisema siku moja: Hakuna Muislamu yeyote atakayefikwa na msiba akasema aliyopendezeshewa na Mwenyezi Mungu kwake kuyasema: "Hakika sisi sote ni wa Mwenyezi Mungu na hakika sisi sote kwake tutarejea" [Baqara: 156], "Ewe Mwenyezi Mungu nilipe" na unipe malipo ya subira yangu "katika msiba wangu", na unipe badala "na unirejeshee" kwa hilo "kheri kuliko hiyo"; isipokuwa Mwenyezi Mungu atampa mbadala bora kuliko hilo. Akasema: Alipofariki Abuu Salama akasema: Ni nani katika Waislamu atakuwa bora kuliko Abuu Salama?! Nyumba ya kwanza iliyohama kwenda kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, kisha mimi Mwenyezi Mungu alinisaidia nikaisema kauli hiyo, Mwenyezi Mungu akanipa badala Mtume rehema na amani ziwe juu yake bora zaidi kuliko Abuu Salama.
Amri ya kuwa na subira wakati wa mitihani masaibu na kutopaparika.
Kuelekeza dua kwa Mwenyezi Mungu katika mambo mazito; kwa sababu kwake ndio kuna mbadala.
Umuhimu wa waumini kutekeleza amri ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake hata isipojulikana hekima yake.
Kheri yote kwa muumini iko katika kutekeleza amri ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake.
Swahiih Muslim (2/ 631) (918).
Imenukuliwa katika vitabu
5 VitabuZaidi (4)
- الذكر والدعاء والعلاج بالرقي من الكتاب والسنة"ما من مسلم تصيبه مصيبة فيقول ما أمره الله، إنا لله وإنا إليه راجعون. اللهم أجرني في مصيبتي، وأخلف لي خيراً منها إلا أخلف الله له خيراً منها" .
- حصن المسلم من أذكار الكتاب والسنةحصن المسلم«إِنَّا لِلَّهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ، اللَّهُمَّ أْجُرْنِي فِي مُصِيبَتِي، وَأَخْلِفْ لِي خَيْرًَا مِنْهَا»[197].
- فتاوى المرضىفتاوى المرضى «ما من مسلم تصيبه مصيبة، فيقول ما أمره الله: إنا لله وإنا إليه راجعون، اللهم أجرني في مصيبتي، وأخلف لي خيرًا منها. إلا أخلف الله له خيرا منها». قالت: فلما مات أبو سلمة، قلت: أي المسلمين خير من أبي سلمة؟ أول بيت هاجر إلى رسول الله صلى الله ع
- مجموعة زاد التربية الإسلامية (2)1«مَا مِنْ مُسْلِمٍ تُصِيبُهُ مُصِيبَةٌ فَيَقُولُ مَا أَمَرَهُ ﷲ: إِنَّا ﷲ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ، اللَّهُمَّ أْجُرْنِي فِي مُصِيبَتِي، وَأَخْلِفْ لِي خَيْرًا مِنْهَا؛ إِلَّا أَخْلَفَ ﷲ لَهُ خَيْرًا مِنْهَا». قالت: «فلما مات أبو سلمة ق