Je anashindwa mmoja wenu kuchuma kila siku mema elfu moja?
Kutoka kwa Saad bin Abii Waqas radhi za Allah ziwe juu yake, amesema:
Tulikuwa kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake, akasema: "Je anashindwa mmoja wenu kuchuma kila siku mema elfu moja?" Akamuuliza muulizaji miongoni mwa waliokuwa naye kwenye kikao: "Vipi anaweza kuchuma mmoja wetu mema elfu moja?" Akasema: "Atasema Sub-haana llahi mara mia moja (100), kisha ataandikiwa mema elfu (1000), au atafutiwa makosa elfu moja (1000)".
كُنَّا عِنْدَ رَسُولِ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَقَالَ: «أَيَعْجِزُ أَحَدُكُمْ أَنْ يَكْسِبَ، كُلَّ يَوْمٍ أَلْفَ حَسَنَةٍ؟» فَسَأَلَهُ سَائِلٌ مِنْ جُلَسَائِهِ: كَيْفَ يَكْسِبُ أَحَدُنَا أَلْفَ حَسَنَةٍ؟ قَالَ: «يُسَبِّحُ مِائَةَ تَسْبِيحَةٍ، فَيُكْتَبُ لَهُ أَلْفُ حَسَنَةٍ، أَوْ يُحَطُّ عَنْهُ أَلْفُ خَطِيئَةٍ».
Maswahaba walimuuliza Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Hivi hawezi mmoja wenu kupata katika kila siku mema elfu moja?! Akasema mmoja kati ya waliokaa naye: Ni vipi atapata mtu mema elfu moja kwa siku kwa wepesi? Akasema: Aseme: "Sub-haana llaah" Yaani: Ametakasika Mwenyezi Mungu, mara mia moja; basi hapo ataandikiwa mema elfu moja; kwa sababu jema moja hulipwa mara kumi mfano wake, au yatafutwa kwake makosa elfu moja.
Himizo la kufanya mazuri; kwa sababu ndio ngazi ya kumfikisha mtu katika utiifu.
Ubora wa kufanya tasbihi (kusema: Sub-haana llaah) na kumtaja Mwenyezi Mungu, na kwamba kazi hii nyepesi ambayo haimgharimu mtu chochote, anapata malipo makubwa kupitia amali hiii.
Hima ya Maswahaba katika kuziendea kheri pasina kuchelewa.
Kuzidishwa kwa mema mpaka mara kumi mfano wake, na hiyo ni kama kauli yake Mtukufu: "Yeyote atakayekuja na jema moja basi atalipwa mara kumi mfano wake" [Al-An'aam:160], na hii ndio daraja ya chini kabisa ya kuzidishiwa, kwani imekuja kuwa ziada hufika mpaka mia saba mara dufu.
Imekuja katika baadhi ya riwaya badala ya (Au) imekuja (Na) katika kauli yake: Au amfutie kwake...Anasema Al-Qaari: Herufi (Wau/na) inaweza kuja ikimaanisha (Au) na riwaya zote hazipingani, maana yake ni kana kwamba: Atakayelisema neno hilo, ataandikiwa mema elfu moja, na asipoandikiwa basi anafutiwa baadhi ya makosa na anachuma malipo kwa sehemu nyingine, na inawezekana kuwa kwa maana ya (Wau/na) au kwa maana ya (Bal/bali) basi hapo atakusanyiwa mambo yote, na fadhila za Mwenyezi Mungu ni pana mno, mwisho wa kunukuu, yaani: Maana yake nikuwa ataandikiwa mema elfu moja na atafutiwa kwake madhambi elfu moja.
Swahiih Muslim (4/ 2073) (2698).
Zaidi (8)
بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين.
لسليم الهلالي (2/ 507).
مرقاة المفاتيح.
لعلي القاري (4/ 1594).
نزهة المتقين شرح رياض الصالحين.
لمجموعة من الباحثين (2/ 980).
مرعاة المفاتيح شرح مشكاة المصابيح.
لعبيد الله المباركفوري (7/ 454).
Imenukuliwa katika vitabu
4 VitabuZaidi (3)
- حصن المسلم من أذكار الكتاب والسنةحصن المسلم«يُسَبِّحُ مِائَةَ تَسْبِيحَةٍ، فَيُكتَبُ لَهُ أَلْفُ حَسَنَةٍ أَوْ يُحَطُّ عَنْهُ أَلْفُ خَطِيئَةٍ»[304].
- رسالة في الأذكار1كنا عند رسول الله صلى الله عليه وسلم فقال: «أَيَعْجِزُ أَحَدُكُمْ أَنْ يَكْسِبَ كُلَّ يَوْمٍ أَلْفَ حَسَنَةٍ؟»، فسأله سائلٌ من جُلَسائه: كيف يكسِب أحدنا ألف حسنة؟ قال: «يُسَبِّحُ مئة تَسْبِيحَةً، فَيُكْتَبُ لَهُ أَلْفُ حَسَنَةً، أَوْ يُحَطّ
- رياض الصالحينرياض الصالحين مع فوائد وهدايات - 7«أيعجزُ أحدُكم أن يَكْسبَ في كلِّ يومٍ ألفَ حَسَنَةٍ!» فسألَهُ سائلٌ من جُلسائه: كيفَ يكسبُ ألفَ حسنَةٍ؟ قَالَ: «يسبِّحُ مائةَ تسبيحةٍ، فيُكْتبُ لَهُ ألفُ حسنةٍ، أوْ يحطُّ عَنْهُ ألفُ خطيئَةٍ».