Skip to content

Hakika amefaulu aliye jisalimisha, na akaruzukiwa kujizuia na kuombaomba, na Allah akamkinaisha kwa kile alichompa

Imepokelewa kutoka kwa Abdallah Ibn Amri -radhi za Allah ziwe juu yao wawili ya kwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake, amesema:

"Hakika amefaulu aliye jisalimisha, na akaruzukiwa kujizuia na kuombaomba, na Allah akamkinaisha kwa kile alichompa".

«قَدْ أَفْلَحَ مَن أَسْلَمَ، وَرُزِقَ كَفَافًا، وَقَنَّعَهُ اللَّهُ بما آتَاهُ».

Imepokelewa Imamu Muslim
Sahihi
Ufafanuzi

Amebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kwamba amefaulu na amebahatika atakayemtii Mola wake akaongozwa na akawezeshwa kuingia katika Uislamu, na akaruzukiwa katika halali kiasi cha mahitaji yake pasina ziada wala mapungufu, na Mwenyezi Mungu akamjaalia kukinai na kuridhika na kile alichompa.

Katika Faida za Hadithi

Utukufu wa mtu upo katika ukamilifu wa dini yake na kupata cha kumtosheleza katika maisha yake na kutosheka kwake na kile alichopewa na Mwenyezi Mungu.

Himizo la kutosheka kwa kile ulichopewa katika dunia ikiwa ni pamoja na Uislamu na sunna.

Rejea

Swahiih Muslim (2/ 730) (1054).

Zaidi (6)

بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين.

لسليم الهلالي (1/ 447).

فيض القدير شرح الجامع الصغير.

للمناوي (4/ 508).

تحفة الأحوذي بشرح جامع الترمذي.

لأبي العلا المباركفوري (7/ 11).