Atakayeswali (wakati) wa baridi mbili ataingia peponi
Imepokelewa Kutoka kwa Abuu Musa Al-Ash'ariy -Radhi za Allah ziwe juu yake- ya kwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema:
"Atakayeswali (wakati) wa baridi mbili ataingia peponi"
«مَنْ صَلَّى الْبَرْدَيْنِ دَخَلَ الْجَنَّةَ»
Mtume rehema na amani ziwe juu yake amehimiza kufanya bidii katika kuswali Swala mbili za nyakati za baridi, ambazo ni sala ya Alfajiri na Alasiri, na akawabashiria kuwa mwenye kutekeleza haki zake kwa muda, na kwa jamaa na mambo mengine, basi zitakuwa ni sababu ya kuingia kwake Peponi.
Fadhila ya kuhifadhi Sala ya Alfajiri na Alasiri; Kwa sababu Alfajiri ni wakati wa usingizi mzuri, na Alasiri ni wakati mtu anashughulika na kazi zake, basi atakayezihifadhi atakuwa na haki zaidi ya kuzihifadhi Swala zilizosalia.
Sala ya Alfajiri na Alasiri zimeitwa baridi mbili; Kwa sababu Swala ya Alfajiri ina ubaridi wa usiku, na Sala ya Alasiri ina ubaridi wa mchana, hata ikiwa ni katika wakati wa joto, ni nyepesi kuliko wakati wa kabla yake, au zimeitwa hivyo kwa kuzingatia kawaida ya nyakati nyingi huwa hivyo, kama ambavyo husemwa: Miezi miwili, kwa kumaanisha jua na mwezi.
Swahiih Al Bukhaariy (1/ 119) (574).
Swahiih Muslim (1/ 440) (635).
Zaidi (4)
نزهة المتقين.
لمجموعة من الباحثين (1/ 159).
شرح رياض الصالحين.
لابن عثيمين (2/ 187).