Skip to content
Orodha ya Sura /

الحُجُرَات

الحُجُرَات is chapter 49 of the Quran and has 18 verses. This page presents it in full in the Uthmani script, with a verse-by-verse translation of its meaning.

18 Aya Sura Na. 49
Nenda kwenye aya
Kiswahili · Barawani
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ لَا تُقَدِّمُواْ بَيۡنَ يَدَيِ ٱللَّهِ وَرَسُولِهِۦۖ وَٱتَّقُواْ ٱللَّهَۚ إِنَّ ٱللَّهَ سَمِيعٌ عَلِيمٞ

Enyi mlio amini! Msitangulie mbele ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia, Mwenye kujua.

Explanation & meanings · 1
  1. Enyi mlio amini! Msitangulie na kulikata jambo lolote la kidini na la kidunia bila ya kukuamrisheni Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Na jiwekeeni kinga ya nafsi zenu isikupateni adhabu ya Mwenyezi Mungu kwa kufuata sharia yake. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia baraabara yote mnayo yasema, ni Mwenye kuyajua vilivyo mambo yote.

يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ لَا تَرۡفَعُوٓاْ أَصۡوَٰتَكُمۡ فَوۡقَ صَوۡتِ ٱلنَّبِيِّ وَلَا تَجۡهَرُواْ لَهُۥ بِٱلۡقَوۡلِ كَجَهۡرِ بَعۡضِكُمۡ لِبَعۡضٍ أَن تَحۡبَطَ أَعۡمَٰلُكُمۡ وَأَنتُمۡ لَا تَشۡعُرُونَ

Enyi mlio amini! Msinyanyue sauti zenu kuliko sauti ya Nabii, wala msiseme naye kwa kelele kama mnavyo semezana nyinyi kwa nyinyi, visije vitendo vyenu vikaharibika, na hali hamtambui.

Explanation & meanings · 1
  1. Enyi mlio amini! Msinyanyue sauti zenu juu ya sauti ya Nabii anapo sema na nyinyi mnasema. Wala msipambanishe sauti zenu na sauti yake, kama mnapo semezana nyinyi kwa nyinyi, kwa kuchelea visiharibike vitendo vyenu bila ya nyinyi wenyewe kutambua.

إِنَّ ٱلَّذِينَ يَغُضُّونَ أَصۡوَٰتَهُمۡ عِندَ رَسُولِ ٱللَّهِ أُوْلَٰٓئِكَ ٱلَّذِينَ ٱمۡتَحَنَ ٱللَّهُ قُلُوبَهُمۡ لِلتَّقۡوَىٰۚ لَهُم مَّغۡفِرَةٞ وَأَجۡرٌ عَظِيمٌ

Kwa hakika wanao teremsha sauti zao mbele ya Mtume wa Mwenyezi Mungu, hao ndio Mwenyezi Mungu amezisafisha nyoyo zao kwa uchamngu. Hao watakuwa na maghfira na ujira mkubwa.

Explanation & meanings · 1
  1. Hakika wanao teremsha sauti zao katika baraza ya Mtume wa Mwenyezi Mungu kwa kumtukuza yeye, hao peke yao ndio Mwenyezi Mungu amezisafisha nyoyo zao kwa uchamngu. Kwa wengineo si hivyo. Nao watapata msamaha mkubwa kufutiwa madhambi yao, na thawabu zilizo fika ukomo wa kufika kwake.

إِنَّ ٱلَّذِينَ يُنَادُونَكَ مِن وَرَآءِ ٱلۡحُجُرَٰتِ أَكۡثَرُهُمۡ لَا يَعۡقِلُونَ

Hakika hao wanao kuita nawe uko nyuma ya vyumba, wengi wao hawana akili.

Explanation & meanings · 1
  1. Hakika hao wanao kuita kwa makelele nawe uko vyumbani mwako wengi wao hawafahamu yanayo takikakana kukuhishimu na kukutukuza kwa makamo yako.

وَلَوۡ أَنَّهُمۡ صَبَرُواْ حَتَّىٰ تَخۡرُجَ إِلَيۡهِمۡ لَكَانَ خَيۡرٗا لَّهُمۡۚ وَٱللَّهُ غَفُورٞ رَّحِيمٞ

Na lau wao wangeli ngojea mpaka uwatokee ingeli kuwa kheri kwao. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye maghfira, Mwenye kurehemu.

Explanation & meanings · 1
  1. Na lau kuwa hao wangeli ngojea, kwa kukufanyia adabu, mpaka ukatoka, bila ya shaka ingeli kuwa ni bora zaidi katika Dini yao. Na Mwenyezi Mungu ni Mkubwa wa kusamehe, Mwenye rehema kunjufu.