50 : 27
۞ قَالَ قَرِينُهُۥ رَبَّنَا مَآ أَطۡغَيۡتُهُۥ وَلَٰكِن كَانَ فِي ضَلَٰلِۭ بَعِيدٖ
Mwenzake aseme: Ee Mola wetu Mlezi! Sikumpoteza mimi, bali yeye mwenyewe alikuwa katika upotovu wa mbali.
Explanation & meanings · 1
- Shetani atasema kumrudi yule kafiri: Ewe Mola wangu Mlezi! Mimi siye niliye mfanya awe mwenye kua'si, lakini yeye mwenyewe alikuwa katika upotovu wa mbali na haki. Na mimi nilimsaidia tu kwa kumpotoa.