50 : 29
مَا يُبَدَّلُ ٱلۡقَوۡلُ لَدَيَّ وَمَآ أَنَا۠ بِظَلَّٰمٖ لِّلۡعَبِيدِ
Mbele yangu haibadilishwi kauli, wala Mimi siwadhulumu waja wangu.
Explanation & meanings · 1
- Hapana la kugeuza kauli ilioko kwangu na onyo langu kuwatia makafiri Motoni, wala Mimi si Mwenye kuwadhulumu waja. Kwani simuadhibu mja yeyote bila ya makosa.